Prof Katundu: Elimu inayotolewa iendane na soko la ajira
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Jamal Katundu
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Jamal Katundu amewasisitiza wakuu wa chuo cha Maji kuhakikisha wamasimamia misingi ya vituo katika kutoa mafunzo, ushauri elekezi pamoja na kufanya utafiti ili kuonyesha vyanzo vipya vya upatikanaji wa maji.
Prof Katundu amesema hayo leo Novemba 2, 2023 jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye mahafali ya 47 ya Chuo cha Maji ambapo jumla ya wahitimu 682 kuanzia ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada wamehitimu katika chuo hicho katika.
Aidha Profesa Katundu amesema ni vyema kukawekwa utaratibu wa vijana wanaohitimu pale tu wanapomaliza wakapatiwa mazingira wezeshi yatakayoweza kusaidia katika ujasiriamali ili kuepukana na tatizo la ajira.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Maji, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk Felician Komu amesema jukumu la chuo hicho ni pamoja na kutoa mafunzo yenye ubora kwa ajili ya kupata wataalamu sambamba na kufanya utafiti katika masuala mbalimbali kuhusiana na maji.