Profesa Lipumba: Ukopaji unaiongeza mzigo Serikali

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba amesema ukopaji wa fedha unaiongezea Serikali mzigo wa madeni.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ,Profesa Ibrahimu Lipumba amesema mjadala unaoendelea kuhusu ukopaji wa fedha kuwa unaiongezea Serikali mzigo wa madeni n ikweli huku akieleza hasa kukopa madeni yenye masharti ya biashara yenye riba za juu.

 Amesema Kuongezeka kwa mikopo ya biashara kumechangia kuongezeka kwa gharama za kuhudumia madeni toka dola 85 milioni mwaka 2010 na kufikia dola 1,198 milioni  mwaka 2020 sawa na Sh2748.5 bilioni  gharama za kulipia madeni ya nje mwaka 2020 ilikuwa sawa na asilimia 15.6 ya mapato ya kodi ya mwaka wa fedha 2019/20.

Akizungumza Dar es Salaam leo  Januari 04,2021 kwenye mkutano wake na vyombo vya Habari, Mwenyekiti huyo amesema ni sahihi kwa serikali inatakiwa kuwa na tahadhari ya mikopo hiyo kwani miaka ya nyuma  nchi ilielemewa na mzigo wa madeni iliyoshindwa kuyalipa kwa wakati  na kuomba kusamehewa madeni hayo.

“Taarifa ya Serikali ya Hali ya Uchumi wa Taifa Mwaka 2020 inaeleza “Sura ya deni imebadilika ambapo mikopo ya kibiashara imeongezeka kufikia asilimia 44.5 ya deni lote la nje mwaka 2019/20 kutoka asilimia 7.2 mwaka 2010/11 na wakati huo huo mikopo ya masharti nafuu ilipungua kufikia asilimia 55.5 kutoka asilimia 92.8 katika kipindi hicho.” Amesema Profesa Lipumba

Katika maelezo yake Profesa Lipumba amesema wanaoibua hoja ya kasi ya ukuwaji wa deni la taifa wasibezwe na badala yake serikali inapaswa kufanyia kazi kwa kukopa mikopo yenye riba nafuu kama walivyochukua mkopo wa dola za Marekani Sh 1.3 trilioni  kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa na kuutumia kuimarisha sekta ya afya, elimu, utalii na kuongeza fedha za kigeni.

Pia amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan Rais Samia  kutumia fungate yake ya kimataifa kutafuta msaada au mkopo usiokuwa na riba toka nchi nje ili kukamilisha miradi ya  kimaendeleo badala ya kubaki kutegemea fedha za ndani zinazotokana na tozo za simu kwani kufanya hivyo ni kuua ujasiriamali kwa wananchi.