Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia aonya udokozi kwenye miradi ya umma

Rais Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa upande wa Tanzania, Dk Patricia Leverley kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma leo Jumapili Oktoba 30, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Spika wa Bunge, Tulia Ackson pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amezindua ujenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Msalato jijini Dodoma ambapo amewataka Watanzania watakaopata fursa za ajira katika mradi huo kuepuka udokozi.

Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania watakaopata fursa za ajira katika ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini hapa kuepuka udokozi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 30, 2022, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa uwanja huo.

Rais Samia amesema mradi huo ni mali ya Watanzania na wakazi wa Dodoma wote.

Rais Samia amewaomba Watanzania kutohujumu mradi huo na badala yake kuwa walinzi wake.

“Wakati mwingine mnapata ajira katika miradi hii lakini mnatabia ya mkono, mkono, kuondoka na mifuko ya saruji, kuondoka na kifuko cha misumari, kipande cha nondo.

“Niombe sana mtakaopata ajira hapa, twendeni tuwajibike ipasavyo ili mradi ukamilike Desemba 2024 wakati ,”amesema.

Amesema ujenzi wa viwanja vya ndege umepewa kipaumbele katika sera ya usafiri nchini ambapo kila mkoa unatakiwa kuwa na kiwanja cha ndege chenye uwezo wa kuhudumia ndege zinazobeba si chini ya abiria 70.

Amesema pamoja na uwanja wa ndege wa Msalato kuna viwanja vya ndege vingine vinaendelea kujengwa nchini.

 Rais Samia amesema lengo lao ni kukuza biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.