Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua bosi mpya Tanroads

Rais Samia ateua bosi mpya Tanroads

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Rogatus Hussein Mativila kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Rogatus Mativila kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Julai 30, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema kuwa Mativila ameteuliwa kuchukua nafasi ya marehemu Mhandisi Patrick Mfugale ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni, 2021.

Kabla ya uteuzi huo Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

Pia, taarifa hiyo imesema kuwa, mkuu huyo wa nchi amemteua Profesa Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico).

Kabla ya uteuzi huo Profesa Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu.

 Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Julai 28, 2021.