Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia awaonya wananchi Kilimanjaro na Uviko-19

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kushangazwa na wananchi Mkoa wa Kilimanjaro, kutochukua tahadhari dhidi ya Uviko- 19, akionya kuwa ugonjwa huo bado upo na wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.

Moshi. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kushangazwa na wananchi Mkoa wa Kilimanjaro, kutochukua tahadhari dhidi ya Uviko- 19, akionya kuwa ugonjwa huo bado upo na wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.

Rais Samia ameyasema hayo leo Ijumaa Oktoba 15, wakati akizungumza na wananchi wa mji wa Moshi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Ushirika (MoCU).

"Nimeingia Mkoa wa Kilimanjaro, nikawa nawaambia wenzangu mbona watu huku hawana habari kabisa na takwimu tulizo nazo Kilimanjaro tumepoteza watu kiasi lakini watu hawana habari wanajitembelea tu hawana barakoa?" amehoji.

Amesema pamoja na kuchanja bado wananchi waendelee kuchukua tahadhari kubwa kwani haya mambo bado yapo.

Ameendelea kusema kuwa takwimu zimeonyesha kuwa chanjo zilizopelekwa mkoa huo zimemalizika na zikaongezwa nyingine na zenyewe zinakaribia kumalizika tena.

“Nawashukuruni sana kwasababu kuchanja kunatupunguzia gharama kubwa sana na gharama za matibabu lakini zinatupunguzia gharama za kupoteza watu wetu ambao ni nguvu kazi ndani ya nchi yetu," amesema Rais Samia.

"Tukikaa bila kuchanja maradhi yakija yanakuja kwa kasi sana, kuchanja kuna saidia," amesema Rais Samia.

 Awali akitoa taarifa ya chanjo mkoani hapa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema mkoa huo unaendelea kutekeleza afua za kupambana na Uviko-19 kama maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya afya, ambapo amesema mkoa huo umemeliza chanjo 60,000 za Jonson & Jonson zilizotolewa awamu ya kwanza.

"Baada ya kumaliza chanjo hizi ilibidi tuombe kuchukua maeneo mengine ambapo tulipewa chanjo dozi 4900 ambazo pia zimekaribia kuisha lakini tayari tumepokea chanjo nyingine 36,864 aina ya Sinopharm," amesema Kagaigai.