Rais Samia kuanza ziara Tanga

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku mbili Mkoa wa Tanga kuanzia kesho Jumapili, Agosti 14, 2022.

  

Tanga. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku mbili Mkoa wa Tanga kuanzia kesho Jumapili, Agosti 14, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Agosti 13, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RC), Omari Mgumba amesema Rais Samia atawasili mkoani humo kesho saa nane mchana.

Amesema atakuwa na ziara ya ziku mbili katika Wilaya ya Mkinga na atazindua Chuo cha Uhamiaji Boma Kichaka miba.

RC huyo amesema kazi nyingine atakayofanya Rais Samia kufunga mafunzo kwa maofisa uhamiaji 818 wanaotarajia kuhitimu mafunzo ya maofisa wa Uhamiaji.

"Niwatake wananchi wa Tanga mjitokeze kwa wingi kumlaki katika maeneo ambayo Rais wetu atapita, ikiwa ni ziara yake ya kwanza aingie madarakani hivyo wananchi tukitokeze kwa wingi.

Rais Samia anafanya ziara Tanga baada ya leo Jumamosi kumaliza ziara mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa aliyoianza Agosti 5, 2022.

Aidha, RC Mgumba amekabidhiwa ofisi hiyo leo na Adam Malima ambaye amehamishiwa Mkoa wa Mwanza.