Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Arusha

Thursday October 14 2021
samiapicc
By Mussa Juma

Arusha. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi siku mbili mkoani Arusha, ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, leo Alhamisi Oktoba 14, 2021 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema Rais atawasili mkoani humo Oktoba 16.

Soma zaidi:Rais Samia kuanza ziara Kilimanjaro kesho

Amesema akiwa mkoani humo, atatembelea mradi wa maji wenye thamani ya Sh520 bilioni uliopo Chekereni wilaya ya Arumeru, pamoja na kuzindua mradi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Engutoto unaojengwa na fedha za ndani za Halmashauri ya jiji la Arusha.

"Baada ya uzinduzi huo Rais Samia anatarajia kuhutubia wananchi katika Uwanja wa Mpira wa Sheikh Amri Abeid "amesema

Mongela amesema Oktoba 18, Rais atazindua Kiwanda cha Nyama Elia Food Overseas LTD kilichopo Namanga  wilayani Longido, atazindua mradi wa maji wilayani hapo pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Advertisement

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi


Advertisement