Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Chalamila atoa ufafanuzi majeruhi ajali ya ndege Bukoba

Waokoaji wakiwatafuta manusura baada ya ndege ya Precision Air iliyokuwa imebeba watu 43 kutumbukia katika Ziwa Victoria Jumapili Novemba 6, 2022.Katika ajali hiyo 19 walifariki dunia huku 26 wakinusurika.

Muktasari:

Ajali hiyo ya ndege imehusisha ndege aina ya ATR 42-500 ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba na ilipotaka kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba iliangukia ziwani, mita 100 kutoka ulipo uwanja wa ndege.

Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RC), Albert Chalamila amesema kati ya majeruhi 26 katika ajali ya ndege ya Precision Air wawili walikuwa waokoaji.

Jana Jumapili, taarifa zilisema watu waliookolewa ni 26 huku vifo vikiwa 19 na kufanya idadi ya watu waliokuwa kwenye ndege kuwa 45 tofauti na idadi ambayo ilitolewa na Shirika la Precision Air na Mkuu huyo wa Mkoa kuwa watu 43 walikuwa kwenye ndege hiyo.

Kutokana na kutofautiana kwa taarifa hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika eneo la ajali aliagiza kufanyika uchunguzi wa idadi kamili ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Leo Jumatatu Novemba 7, 2022, akizungumza katika shunguli ya kuaga miili hiyo katika uwanja wa Katibaba mjini Bukoba, Chalamila ametoa ufafanuzi kuwa watu 24 waliookolewa walikuwa kwenye ndege huku wawili wakiwa waokoaji.

“Walifariki katika ajali ile ni 19, waliookolewa naomba hapa niweke data vizuri, waliookolewa ambao walikuwa wasafiri ni 24 na sio 26 kama tulivyoripoti jana. Lakini kijana mmoja aliyekuwa anaokoa alijeruhiwa” amesema Chalamila

Miongoni mwa majeruhi waliokuwa wakiokoa watu hao ni kijana aliyefungua mlango wa mdege Majaliwa Jackson ambaye amepewa Sh1 milioni kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.