RC Kagaigai kuwashughulikia waliokwama kuwaondoa machinga
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai
Muktasari:
- Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amemwagiza kamanda wa polisi wa mkoa huo kuhakikisha wanachukuliwa hatua wanaokwamisha zoezi la kuwaondoa wamachinga.
Moshi. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amemwagiza kamanda wa polisi wa mkoa huo kuhakikisha wanachukuliwa hatua wanaokwamisha zoezi la kuwaondoa wamachinga.
Kagaigai ametoa maelekezo hayo wakati alipokutana na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri ,makatibu tawala wa wilaya pamoja na Maofisa tarafa wa mkoa huo wakati wa kikao cha kujadili mikakati mbalimbali ikiwemo utekelezwaji wa ujenzi wa madarasa.
"Kuna baadhi ya watu wanaonyesha kukwamisha zoezi hili la machinga na wanafanya kwa 'interest'zao binafsi, suala hili la kuwapanga machinga kwenye maeneo mengine mapya ni kuondoa msongamano huku mjini ni agizo la Rais.
"Yeyote anayepinga na kukwamisha zoezi hili ni mhalifu kama wahalifu wengine RPC katika pita pita zenu na taarifa zenu za kiintelijensia ukisikia kuna mtu anataka kukwamisha huyo ni mhalifu kama mhalifu mwingine,"amesema Kagaigai
Kesho Oktoba 29 zoezi la kuwaondoa machinga hao katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Moshi litaendelea na ambao watakaidi zoezi hilo watachukuliwa hatua za kisheria.