Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Mwassa awatangazia kiama watumishi wabadhirifu

Baadhi ya wakuu wa taasisi za Serikali mkoani Kagera wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa (hayuko pichani) wakiwa wa kikoa cha kupokea na kusikiliza mikakati ya kiutendaji ya taasisi hizo. Picha na Alodia Dominick 

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ametangaza kyama cha watendaji na watumishi wa umma mkoani humo watakaobainika kujihusisha na makosa ya uzembe, uongo, uvivu, ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo na ubadhilifu wa fedha na mali za umma.

Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ametangaza kyama cha watendaji na watumishi wa umma mkoani humo watakaobainika kujihusisha na makosa ya uzembe, uongo, uvivu, ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo na ubadhilifu wa fedha na mali za umma.

Akizungumza wakati wa kikoa chake cha kwanza na viongozi na wakuu wa taasisi za umma mkoani humo Mei 29, 2023, Mwassa ameonya kuwa katika uongozi wake, hatamvumilia kiongozi, mtendaji wala mtumishi yeyote atakayekutwa na makosa hayo matano aliyoyataja kuwa sumu ya maendeleo katika jamii.

"Kagera hatutakuwa tayari kuwa na viongozi, watendaji na watumishi wazembe, waongo, wavivu, wanaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na wanaofuja fedha na mali za umma. Tutawakataa. Tunahitaji watu wachapa kazi watakaouvusha mkoa wetu kutoka hapa tulipo kwenda mbele zaidi,’’ amesema Mwassa aliyehamishiwa Kagera akitokea Mkoa wa Morogoro

Mwassa ambaye ni mwandishi wa habari kitaaluma amewataka viongozi wa wilaya na halmashauri za Mkowa wa Kagera kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kila mmoja katika eneo lake ili kufanikisha lengo la Serikali la kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

Huku akiwageukia viongozi wa Wilaya na Manispaa ya Bukoba, Mkuu huyo wa mkoa ametaja mradi wa ujenzi wa Stendi Kuu mjini Bukoba huk akiahidi kuwa mradi huo ni moja ya vipaumbele vyake.