Ripoti ya CAG yabaini hasara ya Sh35 bilioni ATCL

New Content Item (1)
ATCL yatengeneza hasara ya Sh60 bilioni

Dar es Salaam. Ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) umebaini Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imekuwa ikipata hasara kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo. Pamoja na Serikali kutoa ruzuku ya Sh30.63 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Hayo yamebainishwa na CAG kupitia ripoti yake ya Mashirika ya umma ya mwaka 2021/2022 iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 6, 2023

CAG ameeleza katika ripoti hiyo kuwa ATCL bado iliripoti hasara ya Sh35.23 bilioni

‘’Serikali isingetoa ruzuku hiyo, kampuni ingepata hasara ya Sh65.86 bilioni.  Hii inaonesha changamoto ambazo Kampuni ya Ndege Tanzania inakabiliana nazo katika soko kwa sasa. Hivyo, Kampuni ya Ndege Tanzania itathmini upya mbinu na mikakati ya uendeshaji ili kupunguza gharama na kuongeza mapato’’ Ripoti ya CAG

CAG amebainisha kuwa Mashirika na taasisi zingine za umma ziboreshe ufanisi wa utendaji ili kuongeza ukusanyaji wa mapato na kutekeleza mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji.

“Taasisi zianzishe na kuimarisha mikakati ya kubadilisha mwelekeo wa uwekezaji na uendeshaji wa biashara zisizofanya vizuri, kufanya uwekezaji wenye tija na endelevu ili kuongeza mapato”