Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RPC aliyetamani kuwa IGP achunguzwa

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Tanzania, limemrudisha makao makuu ya jeshi hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Wankyo Nyigesa kupisha uchunguzi kutokana na matamshi aliyoyatoa Machi 26, 2022 katika sherehe za kumuaga wakati akihamishwa kutoka mkoani Pwani kwenda Kagera.

  


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Tanzania, limemrudisha makao makuu ya jeshi hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Wankyo Nyigesa kupisha uchunguzi kutokana na matamshi aliyoyatoa Machi 26, 2022 katika sherehe za kumuaga wakati akihamishwa kutoka mkoani Pwani kwenda Kagera.

Nyigesa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani baadae akahamishiwa mkoa wa Kagera.

Akizungumza katika sherehe za kumuaga wakati akihamishwa Kamanda Nyigesa alisema kuwa anatamani siku moja Rais Samia amuote na kumtamka kuwa IGP wa Tanzania ili akafanye kazi kubwa ya kuleta mabadiliko.

“Mi naomba nifanye miaka mitatu tu halafu baadaye nimwambie mama ‘mimi nakukabidhi naondoka, unaonaje hapo?’” alisema Nyigesa huku watu waliohudhuria hafla hiyo wakiangua vicheko.

Alisisitiza kwamba IGP aliyepo madarakani, Simon Sirro hajafanya makosa, anafanya mambo mazuri lakini yeye atafanya mazuri Zaidi.

“Unajua binadamu lazima utarget ya mbele, kuwa na ndoto kubwa, sasa huwezi kuwa na ndoto kwamba nitaendelea kuwa kamanda, mimi nataka kuwa nafasi hizo, kamishna, IGP ili baadaye nifanye makubwa ambayo nimeyafanya,” alisema Nyigesa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne Machi 29, 2022 na msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza kuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Simon Sirro amesema nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), William Mwampagale

Taarifa hiyo inaeleza kuwa matamshi aliyoyatoa yanaonyesha kuwepo na ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozi ya jeshi hilo.

“Suala hilo limeanza kufanyiwa kazi na matokeo ya uchunguzi huo yatafikishwa katika mamlaka za kinidhamu kwa hatua zaidi” imeeleza taarifa hiyo.

Vile vile, aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Theopista Mallya anakuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), William Mwampagale ambaye amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera.

Taarifa imeeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Operesheni mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Mashenene Mayila anakuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa wa Rukwa.