Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rufiji yatumia Sh90 milioni ya mapato ya ndani ujenzi nyumba za waalimu

Nyumba mpya zilizojengwa kwa ajili ya walimu kuishi Wilayani Rufiji.

Rufiji. Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imetumia Sh90 milioni kwa ajili ujenzi wa nyumba tatu za waalimu kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Hayo yamesemwa leo, Februari 17, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, John Kayombo.

“Kwa kipindi cha mwaka moja na miezi mitano Halmashauri imepeleka zaidi ya Sh495 milioni kwenye idara za elimu kwaajili ya kujenga nyumba 16 na kukarabati nyingine sita ambazo zipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ikiwemo Shule ya Msingi Mbwara ambayo ilikuwa na hali mbaya ya makazi na sasa tumejenga nyumba tatu kwa Sh90 milioni,” amesema Kayombo na kuongeza,

Nyumba za zamani walizokuwa wanaishi walimu Wilayani Rufiji.

“Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji itaendelea kutekeleza nia ya Rais Samia ya kuboresha maslahi na miundombinu ya watumishi kwa kutumia mapato ya ndani kujenga na kuboresha makazi ya walimu pamoja na watumishi wengine ili kuhakikisha wanafanyakazi kwenye mazingira mazuri yatakayoleta tija kwa Maendeleo ya Taifa,”

Pia, Kayombo amesema katika mpango wa bajeti ya mwaka 2023/2024 halmashauri hiyo imepanga kuendelea kuboresha makazi ya waalimu hususani wa maeneo ya vijijini kwa ajili ya kuongeza motisha.

Peter Kwachilu, mdau wa elimu amesema hatua hiyo itasaidia kutoa motisha kwa waalimu na kuongeza ufanisi na ubora kwenye elimu.

"Kila siku tunalia na makazi duni ya waalimu na kutokuwa na motisha, lakini kwa mipango kama hii inasaidia kuongeza ari kwa waalimu hasa wa vijijini," amesema Kwachilu.