Rugemalira afutiwa mashtaka, aachiwa huru

Rugemalira aachiwa huru

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara maarufu Tanzania, James Rugemalira.Dar es Salaam.  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara maarufu Tanzania, James Rugemalira.

Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashataka nchini (DPP) kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya mshtakiwa huyo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuachiwa leo Alhamisi Septemba 16, 2021, Mike Ngalo ambae ni wanasheria wa Rugemalira amesema mteja wake  amefutiwa mashtaka yote baada ya DPP kusema kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Rugemalira aachiwa huru

Rugemalira alikuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akituhumiwa kujipatia fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.