Russia kutumia nyuklia Ukraine

Rais wa Russia, Vladimir Putin

Muktasari:

  • Baada ya mapigano kudumu kwa zaidi ya miezi saba sasa, Rais wa Russia, Vladimir Putin ametangaza uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia jambo linaloonekana kuwa la hatari kwa Umoja wa Ulaya (EU) na washirika wake.

Moscow, Russia. Baada ya mapigano kudumu kwa zaidi ya miezi saba sasa, Rais wa Russia, Vladimir Putin ametangaza uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia jambo linaloonekana kuwa la hatari kwa Umoja wa Ulaya (EU) na washirika wake.

Hofu hiyo inakuja wakati Russia ikihamasisha kuhamishia vita katika mikoa minne ya Ukraine.

Putin amekabiliwa na vikwazo katika uwanja wa vita, huku vikosi vyake vikirudishwa nyuma nchini Ukraine.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) juzi, Mkuu wa Sera za Kimataifa wa EU, Lyse Doucet alisema matumzi ya silaha za nyuklia ni hatari.

“Hakika ni wakati hatari kwa sababu Jeshi la Russia limebanwa, na majibu ya Putin kutishia kutumia silaha za nyuklia ni mabaya sana,” alisema Doucet.

Ni miezi saba sasa tangu Russia ilipoivamia Ukraine hapo Februari 24 na wachambuzi wanaona majeshi ya nchi hiyo hayajafanikiwa kukamilisha malengo iliyojiwwekea wakishauri suluhisho la mgogoro huo lifanywe kidiplomaisa vinginevyo vinaweza kumalizika lakinikusiwe na amani au vikaibuka vita vingine.

Katika hotuba yake mapema wiki hii, Putin aliieleza nchi yake kuwa ina silaha mbalimbali za uharibifu na itatumia njia zote zinazowezekana akisisitiza kuwa “sidanganyi.”

Tamko la Rais Putin limetolewa wakati akiwa ametia saini agizo la kuhamasisha wananchi kujiunga na jeshi kwenda kuongeza nguvu vitani nchini Ukraine.

Jambo hilo linaelezwa kuwa la kwanza katika historia ya nchi hiyo na haitabiriki litaleta mafanikio ya aina gani.

Jambo hilo limefanyika kulingana na sheria pamoja na amri ya Putin na taarifa ya Waziri wa Ulinzi, Sergei Shoigu.

Kwa mujibu wa sheria ya mafunzo na uandikishaji watu ya nchi hiyo, wananchi walioko katika kikosi cha akiba ni wale ambao hawana rekodi ya uhalifu ambayo haijaisha au wenye rekodi ya uhalifu mkubwa ambayo haijaisha muda wake wataandikishwa kulitumikia jeshi.

Putin amesema uandikishaji huo utawahusu “hasa wale ambao wametumikia katika safu ya jeshi, wana taaluma fulani za kijeshi na uzoefu unaofaa.”

Uamuzi wa kukusanya watu uliamriwa kutokana na hitaji la kuimarisha safu ya mapigano kati ya askari wa Russia na Ukraine.

Kikosi cha akiba pia kinajumuisha ile inayoitwa ukusanyaji wa watu wa akiba ambao ni askari wa akiba ambao wametia saini mkataba na Wizara ya Ulinzi.

Kulingana na masharti, watashiriki mazoezi ya kijeshi na mikutano, kupata mshahara wa wastani na kupokea malipo ya ziada, na katika kesi ya tamko la sheria ya kijeshi, kwa uhuru wao wataenda katika kitengo cha kijeshi walichopangiwa.

Wakati Russia ikiendelea na mipango hiyo, China na India on Satzimeuomba Umoja wa Mataifa kuratibu mazungumzo ya kidiplomasia kuvimaliza vita vinavyoendelea kati yake na Ukraine.

Baada ya juma zima la kutaka kusitishwa kwa vita hivyo kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alizikemea nchi za magharibi kwa kile alichokiita upotoshaji wa makusudi unaofanywa dhidi ya Warussia ingawa mpaka sasa hakuna Taifa lolote lililoiunga mkono Russia ikiwamo China ambayo siku chache kabla ya kuanza kwa vita hivyo ilisema ushirikiano wake na Russia hauvunjiki.

Katika tamko lake, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi aliziomba Russia na Ukraine kuweka silaha chini ili kuepusha mzozo huo kuenea mpaka kwenye mataifa mengine jambo litakaloziathiri zaidi nchi masikini.

“China inaunga mkono juhudi zozote za kupata muafaka wa mgogoro huu. Jambo muhimu kwa sasa ni kuwezesha mazungumzo,” alisema Yi ambaye ameshakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba.

Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Subrahmanyam Jaishankar alisema kadri vita hivyo vinavnavyoendelea wamekuwa wakiulizwa wanamuunga nani mkono na “majibu yetu mara zote yamekuwa bayana, India inaegemea kwenye amani na itaendelea kubaki hapo. Tupo upande unaotaka mazungumzo yafanyike.”