Ruto Rais mteule Kenya

William Ruto

Muktasari:

Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati imemtangaza mgombea wa Kenya Kwanza, William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya.

Nairobi. Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati imemtangaza mgombea wa Kenya Kwanza, William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya.

Ruto ambaye ni Naibu Rais wa Kenya, ameshinda uchaguzi huo uliokuwa na mchuano mkali kati yake na mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga aliyekuwa akipigiwa debe na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

#LIVE: Ruto Rais mteule Kenya

Leo Jumatatu Agosti 15, katika ukumbi wa Bomas uliokuwa ukitumika kwa ajili ya kuhakiki kura za urais, Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ametangaza matokeo hayo baada ya siku sita za kihoro cha kuyasubiri tangu siku iliyopigwa kura.

Ruto amewashinda wagombea wenzake Raila Odinga, mgombea wa Chama cha Agano, David Waihiga ambaye alitangaza jana kushindwa na Profesa George Wajackoyah wa Chama cha Roots.

Matokeo ya urais kwa wagombea wote kwa asilimia ni kama ifuatavyo;


William Ruto-50.49 %


Raila Odinga- 48.85 %


David Waihiga- 0.23 %


George Wajackoyah-0. 44