Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu kifo cha Balozi Kijazi

Sababu kifo cha Balozi Kijazi

Muktasari:

  • Katibu mkuu  ofisi ya rais utumishi, Dk Laurean Ndumbaro amesema aliyekuwa katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.

Dar es Salaam. Katibu mkuu  ofisi ya rais utumishi, Dk Laurean Ndumbaro amesema aliyekuwa katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.

Balozi Kijazi alifariki dunia Februari 17, 2021 jijini Dodoma katika hospitali ya Benjamin Mkapa na mwili wake uliagwa jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na leo Jumamosi Februari 20, 2021 inafanyika ibada ya mazishi wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga.

Akizungumza katika ibada hiyo, Dk Ndumbaro amesema Balozi Kijazi aliugua kwa muda mfupi na kufikishwa katika hospitali ya Mkapa kwa matibabu.

“Balozi John Kijazi aligua kwa muda mfupi ambapo Februari mosi, 2021 alilazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma ambapo amekuwa akitibiwa hadi mauti ilipomfika usiku wa Februari 17, 2021. Balozi amefariki kwa maradhi ya moyo yaani akiwa na umri wa miaka 64,” amesema Dk Ndumbaro.

Akieleza wasifu wa marehemu, Dk Ndumbaro amesema Balozi Kijazi aliteuliwa na kupandishwa cheo kuwa katibu mkuu kiongozi na katibu wa baraza la mawaziri Machi 6, 2016 nafasi aliyoitumikia kwa weledi na uadilifu mkubwa hadi umauti ulipomkuta.

Sababu kifo cha Balozi Kijazi

 “Balozi Kijazi alistaafu Novemba 14, 2016 lakini kutokana na umahiri wake wa kazi, Rais John Magufuli alimwongezea ajira ya mkataba hadi umauti ulipomkuta. Katika maisha yake ya ndoa alijaliwa kupata watoto watatu ambao ni David, Emmanuel na Richard, mke na wajukuu wawili,” amesema Dk Ndumbaro.

Amesema Balozi Kijazi aliteuliwa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Agosti 21, 2020 na Desemba 17 alishiriki kwa mara ya kwanza mahafali ya 11 ya chuo hicho.

Sababu kifo cha Balozi Kijazi

Amesema Balozi Kijazi aliwahi kupata tuzo ya mfanyakazi bora Mkoa wa Kilimanjaro mwaka 1984, 1989 na mwaka 1991 akiwa mkoani Lindi.

Kwa upande wa taaluma, Dk Ndumbaro amesema Balozi Kijazi alikuwa amesajiliwa na Bodi ya Wahandisi kama mhandisi mtaalamu.