Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ya kuahirisha hukumu kesi ya Membe, Musiba yatajwa

Sababu ya kuahirisha hukumu kesi ya Membe, Musiba yatajwa

Muktasari:

  • Hukumu ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe dhidi ya mwanahabari anayejitambulisha mwanaharakati huru, Cyprian Musiba imepigwa kalenda hadi Oktoba 28, 2021.

  


Dar es Salaam. Hukumu ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe dhidi ya mwanahabari anayejitambulisha mwanaharakati huru, Cyprian Musiba imepigwa kalenda hadi Oktoba 28, 2021.

Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe anamdai Musiba fidia ya jumla ya Sh10.3 bilioni kwa madai ya kumkashfu, kupitia magazeti yake ya Tanzanite.

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa itolewe leo Jumanne Oktoba 12, 2021 na Jaji Joaquine De Mello imeahirishwa kwa sababu haijakamilika kuandikwa.

Wakili wa Membe, Jonathan Mndeme amesema hukumu hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 kwa kuwa Jaji De Mello bado hajamaliza kuiandika.

Mbali na Musiba, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa Gazeti la Tanzanite linalomilikiwa na Musiba, na kampuni  ya Tz Information and Media Consultant Ltd.