Sabaya aanza kutoa ushahidi akieleza alivyokamatwa

Tuesday January 18 2022
sabaya pic

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (aliyevaa shati nyeupe) akiwa mahakamani.

By Janeth Mushi

Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (35) ameanza kujitetea katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 inayomkabili na wenzake sita.

Sabaya ameanza kujitetea leo Januari 18, 2022 mchana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya mke wake, Jesca Thobias (28) kumaliza kutoa ushahidi wake kwa kumaliza kuulizwa maswali ya dodoso na mawakili watano wa Jamhuri wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule.

Sabaya ameanza kujitetea kwa kuhojiwa na Wakili anayemtetea Mosses Mahuna ambapo mbali na Sabaya watuhumkwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

SOMA:Mke wa Sabaya amaliza kutoa ushahidi kesi ikiahirishwa kwa muda

Hata hivyo, Sabaya hakumaliza kujitetea ambapo Hakimu Patricia Kisinda aliahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo mshitakiwa huyo ataendelea kujitetea mahakamani hapo.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano, la kwanza wakidaiwa wote saba Januari 22, 2021 ni kuongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote saba  wanadaiwa kupata Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso, huku wakijua kupokea fedha hizo ni zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Advertisement

Kosa la pili, tatu na nne Sabaya peke yake ameshitakiwa kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua Sh90 milioni matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.


Mahojiano baina ya Wakili Mahuna na Sabaya yalikuwa kama ifuatavyo;


Wakili: Hebu isaidie mahakama majina yako

Shahidi: Lengai Ole Sabaya

Wakili: Unajishughulisha na shughuli gani

Shahidi: Nilikuwa Mkuu wa Hai, Kilimanjaro

Wakili: Uliteuliwa lini na nani kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai?

Shahidi: Niliteuliwa 29.7.2018 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakili: Na baada ya kuteiliwa ulihudumu kwa nafasi hiyi kwa muda gani?

Shahidi: Miezi 32 kuanzia 2018 hadi Mei 13, 2021 

Wakili: Sababu gani ilifanya wewe usiendelee kuhudumu kwenye nafasi hiyo?

Shahidi: Nilipata taarifa uteuzi huo umesimamishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakili: Je hilo lilikuwa na maana gani?

Shahidi: Maana ya kwamba nimesimamishwa hadi kile ambacho sababu za kusimamishwa zingefahamika.

Wakili: Pengine kwa haraka unaweza kutueleza baadhi ya majukumu yako kama DC Hai?

Shahidi: Kusimamia shughuli zote za ulinzi na usalama kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya wilaya husika,kutatua migogoro yote ya wananchi ya aina yoyote ambayo ipo ndani ya wilaya husika. 

Wakili: Nani ndo boss katika wilaya na mkoa?

Shahidi: Ndani ya wilaya mimi ndiye bosi na ndani ya mkoa, mkuu wa mkoa ndiye bosi

Wakili: Siku ya 22/1/2021 wewe ulikuwa wapi na ulikuwa ukifanya nini tangu asubuhi hadi jioni?

Shahidi: 22.1.2021 niliondoka saa 1:30 nikaenda ofisini na nilifuatwa na dereva na gari ya Serikali, ofisi hizo ziko Bomang'ombe wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, nikatatua mgogoro wa wafugaji na wakulima walikuja saa 3 mpaka saa 11 kasoro jioni.

Na siku hiyo mgogoro huo nilitatua mimi na msaidizi wangu mkuu ambaye ni DAS anayeitwa Upendo Wella na baada ya mgogoro kuisha saa 11 nikaondoka kurudi home kwangu kwenye makazi ya DC Hai na ilikuwa siku ya ijumaa jua lilikua lianazama sabato ikaingia

Wakili: Uliposema majira ya jioni Sabato iliingia ulikuwa unamaanisha nini?

Shahidi: Mimi ni mkristo dhehebu la Sabato na kwa mujibu wa desturi ya dhehebu ikifika jioni jua likizama sabato inaingia tunafanya maandalizi ya imani

Wakili: Unasema majira ya asubuhi saa moja na nusu ulimuaga mke wako huyo mke wako wanaitwa nani

Shahidi: Mke wangu anaitwa Jesca Thomas Nassari

Wakili: Huyu mke wako Jesca ulifunga nae ndoa lini?

Shahidi: Nilifunga nae ndoa 27/5/2018 katika katika la Waadventista Sabato Arusha (Central)

Wakili: Ulizungumza habari ulifuatwa na dereva aliyekuwa na gari huyu dereva anaitwa nani na alikufuata na gari gani kukupeleka kazini?

Shahidi: Dereva huyo anaitwa Thobias Kivuyo wa Serikali na alinifuata na gari ya serikali Land Cruiser V8 lenye namba za usajili STK, namba za mbele sikumbuki lakini sikumbuki kwa uhakika inaishia na 42.

Imesajiliwa hazina na ipo kwenye registry ya mkoa wa Kilimanjaro kama gari iliyokuwa assignened kutumika na DC Hai

Wakili: Umesema gari hii imesajiliwa hazina na inapatikana kwneye registry ya mkoa wa Kilimanajaro kama gari ya nani?

Shahidi: Gari iliyokuwa assigned kutumika na Mkuu wa wilaya ya Hai

Wakili: Umesema hii gari usajii wake ni STK na usajili wake ni imeishia 42 kwsninu hukumbuki hizo nyingine?

Shahidi: Gari inaposajiliwa anakabidhi gari kwa DAS na anamkabidhi gari dereva,matumizi ya gari inakwenda wapi, maintanance ya gari na vitu vyote kuhusu gari anayepaswa na anayefahamu ni dereva

Wakili: Sasa huyu dereva wako pale wilayani anakua chini ya usimamizi wa nani au hata huko mkoani?

Shahidi: Dereva wilayani anasimamiwa na DAS ambaye anampa mafuta na aanasimamia safari zote na mkoani anasimamiwa na katibu msaidizi rasilimali watu

Wakili: Kwa uelewa wako unaweza kueleza mahakama hii utaratibu wa gari ya DC kutoka na dereva kuelekea mahali popote ndani ya wilaya, mkoa na nje ya mkoa ukoje?

Shahidi: Dereva ni mwajiriwa wa Serikali na gari ni mali ya serikali,ili dereva atoke sharti la lazima ni lazima iwe imeratibiwa na DAS ambaye ni lazima amjulishe afisa msaidizi wa rasilimali watu mkoa na kama ni safari ya nje ya wilaya ni lazima kuwe na kibali ambacho kinatolewa na ofisa rasilimali watu wa mkoa na kuidhinisha gari kutoka ambaye anamjulisha DAS na inatika kwa sababu ipi na sababu hizo zinaainishwa na kuandikwa na baada ya hapo lazima DAS atoe idhinisho la maandishi kwa dereva kwani yeye ndiyo anaidhinisha na kutoa mafuta na kama itatokea kinyume chake dereva akitoka sharti dereva aadhibiwe kwa kujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazomuongoza na ionyeshwe ameadhibiwa

Wakili: Hebu ieleze mahakama utaratibu wa wewe DC kutoka nje ya kituo chako cha kazi lakini umo ndani ya mkoa na utaratibu wa kutoka nje ya mkoa ukoje?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu utaratibu wa kutoka wilaya nyingine unamtaarifu Mkuu wa Mkoa na kama ndani ya mkoa unaweza kumtaarifu kwa njia ya simu au barua.

Nje ya mkoa ni lazima uombe ruhusa kwa kueleza sababu,na utoe taarifa siku saba  kabla ya kwenda huko unakotaka kwenda na RC akubali kwa maandishi kwamba nimekuruhusu na ikitokea kinyume chake hukafanya hivyo lazima RC atakuandikia barua ya kutaka maelezo ukieleze kwanini isichukuliwe hatua kwa kukiuka sheria taratibu na miongozo na kutokuwepo kwenye kituo cha kazi bila ruhusa

Wakili: Sabaya hebu ieleze mahakama huyu Thobias kwa sasa huyo wapi?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu Thobias Kivuyo yuko wilaya ya Hai?kilomita 45 toka hapa tulipo ni mwajiriwa wa Serikali mpaka 13/5/2021 alikuwa akimuendesha DC Hai

Wakili: Huyo Kivuyo ushahidi wake hapa mahakamani aliutoa lini?

Shahidi: Huyu dereva hajawahi kuja mahakamani kutoa ushahidi


Wakili: Hilo gari la DC lenye namba STK linaishia 42 ni lini liliwahi kutolewa kama kielelezo hapa mahakamani?

Shahidi: Sikimuona derava,sikuiona gari hilo kama kielelezo hapa mahakamani

Wakili: Hapa mahakamani bwana Lengai alikuja mtu kama shahidi namba moja  upande wa jamhuri Renatus Msangila alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Kilimanjaro na anasema katika muda wake wote wa kufanua kazi hakuwahi kupokea barua  toka kwa DAS kuwa Januari 22, wala dereva wako wala gari lilitoka nje ya mkoa,wewe una nini la kusema?

Shahidi: Ni kweli alisema na asingeweza kupokea kwa sababu sikutoka,shahidi huyo alieleza hakuna namna dereva na gari zitatoka bila yeye kufahamu mpaka anatoa ushahidi wake 18/9/2021 alisema hana taarifa dereva ametoka wala gari yake na amethibitisha hata Das alisema hana taarifa za dereva wala dc wala gar kutoka wilaya ya Hai nje ya kituo cha kazi na alisema yeye ndo msimamizi wa nidhamu wa dereva na hadi siku anatoa ushahidi na hajachukua hatua kwa dereva kwa sababu hakutoka

Wakili: Lengai kwa uelewa wako kama DC ambaye amesimamishwa unafikiri kwanini Renatus alisema kwamba endapo wewe au dereva gari au wewe yeye angeoaswa kufahamu kwanini yeye hafahamu?

Shahidi: Alikiwa ofisa rasilimali watu msaidizi na custodiam wa mali za mkoa.

Yeye ni msimamizi mkuu wa watumishi na mtu akitoka lazima yeye msimamizi mkuu afahamu na yeye ndiye msimamizi mkuu wa ligistics za hao watu kutoka na gari likitoka lazima yeye awe anafahamu ndo anaidhinisha namna ya gari kutokaWakili: Hapa alikuja shajidi wa 13 wa jamhuri anaitwa Ramadhan Juma,yeye ni mchunguzi wa Takukuru na alieleza mahakama yeye ndiye mchunguzi mkuu anasema katika ushahidi wake 22/1/2021 wewe pamoka na gari ya serikali yenye namba STal 5434 mlitoka nje ya mkoa wa Kilimanjajro kuja Arusha wewe unalizungumziaje?

Shahidi: Mheshimiwa Hakkimu nimeeleza gari ya serikali lilikuwa namba STK inaishia 42, shahidi wa 1 ameeleza hakuna namna gari dereva wala mimi shahidi wa 13 ni muongo.

Shahidi huyo hajajaribu hata kuleta registry ya mkoa ni mali ya Kilimanjaro ni kwa sababu haipo ni muongo shahidi huyo hajaleta hiyo gari.

Angeleta hiyo gari hapa mahakamani shahidi huyo amedai tu kwa maneno kwamba ameona log book kuna mtu alitoka hai,hajaleta hiyo logbook ambayo amesema ipo.

Shahidi huyo amesema anamfahamu dereva,ameshindwa kumleta mwendeshaji wa hiyo gari athibitishe tu ya kwamba ulikuwa na safari hiyo.Huyo ni shahidi muhimu kuliko mdhamini wa ndoa

Wakili: Wewe bwana Lengai unatuambia hapa mahakamani gari DC Hai ni STK inayoishoa 42 hali kwamba shahidi pekee aliyezungumza gari ya DC Hai ni huyu shahidi wa 13 kuwa STL5434 wewe hili unalizungumziaje?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu ushahidi wa gari unatakiwa uletwe na uthibitisho ili kutoacha mashaka

Mashkata umeleta gari walilosema wamekatama Dar Es Salaam kilomita 609 na wameleta mashahidi  wa 6, 8, 11 na 12 wote wametoka Dar mpaka  hapa mahakamani kuileta gari iliyopo Hai kilomita 45 au kuleta dereva kumewashinda nini ambaye aliiendesha gari hiyo kuthibitisha shtaka kubwa namna hii.

Kwa sababu hiyo gari haipo  

Wakili: Unamfahamuje mtu anaitwa Francis Mroso?

Shahidi: Simfahamu mheshimiwa nimemsikia kwa mara ya kwanza hapa mahakamani kama shahidi wa 10 na kumuona

Wakili: Unamfahamu vipi mtu anaitwa Adanbest Marandu?

Shahidi: Mhe hakimu sijawahi kumsikia wala kumuona mtu huyo kwa mara ya kwanza nilimuona kama shahidi wa tatuhapa mahkamani

Wakili: Na je unamfahamuje mtu anayeitwa Philemon Kazibila?

Shahidi: Mara ya kwanza alikuja kama shahidi wa nne ndo nilimuona 

Wakili: Je unamfahamuje mtu anaitwa Juma Nuhu?

Shahidi: Kwa mara ya kwanza nimemsikia hapa alivyokuja kama shahidi namba tano

Wakili: Bwana Lwngai hap mahakamani wamekuja mashahidi wanne Marandu, Kazibila, Nuhu na Mrosso na hawa mashahidi wote kwa pamoja wanasema 22/1/2021 majira ya mchana kuanzia saa nane  wao walikuona katika eneo la Mrosso lililopo Mbauda na wao wanasema kilichowafanya wakutambue wewe ni kwa sababu wanakuona kwenye TV na social media wewe unajiteteaje juu ya hilo?

Shahidi: Hao watu walidai hivyo hapa mahakamani wote ni waongo wka sababu mimi nilikiwa siku hiyo Bomang'ombe, Hai ofisini lakini mheshimiwa Hakimu hao mashahidi wote wamedai ndiyo mara yao ya kwanza ukiacha Mroso walidi ndo mara yao ya kwanza kuniona na wamekuwa wkainiona kupitia TV

Upande wa mshtaka haukujiangaisha kufanya gwaride la utambuzi ili akatbihitishe huyo mtu aliyemuona ni yeye.

Hao ni mashahidi waongo na ndio manaa hata shahidi wa 3 alisema alimuona mtu kama Sabaya hana uhakika na huyo Sabaya wa kwenye TV ni mimi

Wakili: Unasema mashahidi hao si wa kweli iweje shahidi namba tatu ambaye ni mlinzi kwa Mrosso aandikishe kitabu cha getini no za gari Stl 5434, T 144 CZU na T 446 CTU ambazo shahidi wa 13 anasema ni zako na ulitumia kwenda kwa Mrosso?

Shahidi: Uthibitisho wa gari kuwa ya mtu sio maneno, mmiliki wa gari sio maneno ni zile nyaraka zilizopatikana kwa njia halali, zimetajwa gari tatu hata kuileta moja hazijaletwa na ni zangu

Kwanini wanauzia vielelezo vingine, vingine wanavitoa hapo kuna nini?

Hitimisho lake ni kwamba hizo gari hazipo na kama hazipo zisingeweza kwenda Mbauda

Wakili: Amekuja hapa shahidi namba sita James Wawenje Vodacom PLC, alitaja namba za simu 0758 707171 wewe Lengai unaifahamu vipi hiyo namba

Shahidi: Hiyo namba ya simu ni namba ambayo anaitumia mke wangu Jesca kwenye shughuli zake za ujasiriamali na biashara ndogondogo anazofanya.

Na namba hiyo siyo ya kwangu, siyo ninayotumia kwa matumizi yangu binafsi na walimkuta nayo walipomkamata walipovamia maofisa wa Takukuru na wengine wa Polisi, walimkuta Jesca Thomas na simu aina ya Samsung ambayo ndani yake ina hiyo namba na wakaichukua na wanajua

Wakili: Bwana Lengai Ole Sabaya siku ya tarehe 22/1/2021 ni nani alikuwa na laini hiyo ya simu na ni nani alikuwa akiitumia kufanya mawasiliano?

Shahidi: Mke wangu Jesca ndo alikuwa akitumia namba hiyo na aliyekuwa anafanya mawasiliano kwa simu hiyo.

Jamhuri wanasema hiyo ni namba yangu na kielelezo ambacho kimeletwa na Jamhuri kinachoitwa mkataba wa Sabri na Sabaya wa kuuziana gari Lengai Ole Sabaya 0623 550000 ndo namba imeandikwa ni yangu

Wakili: Shahidi namba sita wa Vodacom aliieleza mahakama hajaja kuthibitisha uwepo wa mtu kwenye eneo bali amekuja kuonyesha mnara ambao ‘signal’ ya simu ilipokelewa na sio location ya mtu ila shahidi wa 13 ofisa upelelezi anakuja hapa akisema ulikuwepo Arusha na hata ‘phone record’ inathibitisha uwepo wakati katika maneo tajwa Arusha una nini cha kujitetea?

Shahidi: Tatizo lilianzia kwa shahidi wa 13 ambaye ni mtaalamu wa maendeleo ya jamii kuchambua taarifa za mtaalamu wa voda wa kimtandao ambazo zinataka utalaamu wa masuala ya kisayansi

Mwenye utaalamu wake shahidi wa sita anasema mnara uliosoma ni huu na hakusema siyo location inayothibitisha mtu yupo hapo, lakini asiye na utaalamu huo shahid 13 anadai ameona kielelezo ameona mtu na siyo mtaalamu.

Shahidi 13 ambaye si mtaalamu anayesema simu ilipo ndo mtu alipo haelezi simu yangu haisomi iko gereza la Kisongo nilipo badala yake zipo Takukuru

Wakili: Bwana Lengai kama utakua na kumbukumbu nzuri hebu ieleze mahakama wewe Mei 27, 2021 ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa Dar es Salaam nikiendele na shughuli zangu binafsi nikiwa na mke wangu.

Majira ya saa  10 usiku tukiwa na mke wangu hotelini chumbani Mbezi, tulivamiwa na watu baada ya kugonga sana wakaingia ndani kwa kuvunja dirisha, ambapo wawili waliingia na mmoja akafungua mlango wakaingia wenzao.

Nikawahoji kuna shida gani wakadai ni maofisa wa Takukuru na Polisi wakapeukua chumba kizima, vitu tulivyokuwa navyo na alivyokua navyo Jesca na wote walikuwa wanaume wakiwa na silaha za moto wakatuambia mnatakiwa mkae chini wakafanya upekuzi.

Na baada ya kukusanya baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo wakatuelekeza kushuka chini nikawaeleza nina gari yangu nataka kujua mnanipeleka wapi wakaniambia ofisi za Takukuru, Upanga.

Wakauliza ufunguo wa gari, mtu ambaye nilikuja kumuona hapa mahakamani Shaban, nikamwambia iko kwenye pochi ya Jesca akaenda akachukua ufunguo wa gari hiyo akakuta hela kwenye pochi, akasachi akaziweka pembeni.

Nilipofika Upanga nikakutana na mtu anaitwa bwana Maembe ambaye aliniambia Sabaya unatuhumiwa, lakini utajua tuhuma zako baadaye.

Nikamuuliza kama natuhumiwa ndo mje kutupekua usiku hamna ‘search warrant’, hamna kibali cha kuingia eneo la watu na ni sheria kwamba mnapompekua mtu usiku kabla ya jua kuchomoza na baada ya jua kuzama lazima muwe na kibali cha mahakama hamna sasa mnatafutaje haki ya mtu anayenituhumu huku mkivunja sheria.

Wakanisafirisha usiku Juni 3 kuja Arusha baada ya kukaa ofisi za Upanga siku saba na siku ya 8 nikakaa ofisi ya Takukuru Arusha chini ya kizuizi na kuletwa mahakamani Juni 4, 2021 na kushitakiwa makosa hayaWakili: Bwana Lengai ulikaa ofisi za Takukuru muda gani kabla ya kuletwa Arusha?

Shahidi: Siku nane bila kuambiwa sababu za kunishikilia siku nane kinyume cha sheria na maofisa hao wa Takukuru, mlolongo wote tangu nimekamatwa ni uvunjaji wa sheria hauna tofauti na unyang'anyi na udhalilishji wa wanawake.

Wakili: Kwanini unasema uvunjwaji wa utaratibu tangu unakamatwa?

Shahidi: Maofisa wa Takukuru na Polisi wameingia kwenye makazi ya watu saa 10 usiku na kwa mujibu wa sheria jua kama halijachomoza na sheria inamlazimisha ofisa anayeingia makazi ya mtu usiku kupata kibali cha mahakama ili afanye upekuzi, ni kifungu cha 40 cha Sheria ya CPA.

Wameingia ndani watu wamenisachi na mke wangu, kwa mujibu wa sheria hiyo inamlazimisha mtu anayepekua awe na search warrant. Wakavunja Sheria hiyo tena kifungu cha 38. Sheria inataka ukinisachi umpelekee hakimu taarifa ya kile ulichokikuta kwenye upekuzi kif 38(2) wamevunja ya CPA.

Kitu kingine ambacho maofisa hao walipaswa kufanya baada ya upekuzi ni kutoa risiti palepale walipofanyia upekuzi lakini hawaķufanya kinyume na sheria hiyo kifungu cha 38(3) wakakanyaga na hiyo.

Wakili: Hapo Mbezi hotelini ni watu wangapi walikamatwa?

Shahidi: Walikamatwa watu wawili waliovamiwa, nilikuwa na Jesca chumbani peke yetu

Wakili: Kwa kumukumbu yako vitu gani vilikamatwa?

Shahidi: Hao watu walibeba gari yangu V8 T 222 BDY, walininyang'anya simu zangu mbili, hawa watu walininyang’anya sehemu ya fedha tulizokuwa nazo zilizokuwa kwenye pochi ya mke wangu Jesca, walichukua simu mbili za mke wangu, silaha yangu aina ya pisto.

Maķabrasha yenye nyaraka zangu mbalimbali binafsi, Ipad, Iphone, nikashangaa wakachukua pochi ya mke wangu Jesca na kanga zake, nguo zake na mali zingine.

Wakili: Sasa bwana Lengai kati ya vitu vyote ni vipi ambavyo vimeletwa hapa mahakamani kama vielelezo au uthibitisho wake wa kukamatwa vimeletwa mahakamani?

Shahidi: Ni gari peke yake T 22 BDY, ambayo nimeiona mahakamani hapa 

Wakili: Ni lini wewe ulielezwa kwanini umekamatwa?

Shahidi: Kwa mara ya kwanza nimesikia mashitaka yangu 4/6/2021 nikisomewa mahakamani. Na nikagundua kumbe kuna haki nyingine ya kwangu ambayo ilikiwa imevunjwa kwa mujibu wa sheria

Wakili: Haki gani hiyo

Shahidi: Kwa kuwa nilikamatwa na walionikamata walijua nina mashitaka hayo kwa mujibu wa Sheria nilipaswa ndani ya saa 48 nipelekwe kwenye mahakama ya jirani nilipokamatiwa ndani ya Tanzania Bara.

Wakili: Sasa alikuja shahidi wa 11 alieleza mahakama wakati anakukamata kule Mbezi alikukamata na watu wengine wengi tu ambayo idadi yao hakuitaja wewe unazungumzIje hilo?

Shahidi: Ni aibu kwa ofisa wa Takukuru kusema uongo mahakamani nimevamiwa chumbani nikiwa na mke wangu wawili, ni hotelini utasemaje chumba kingine kulikuwa na watu? Sikuona mtu yoyote aliyevamiwa siku hiyo kuhusu hao wengine ni uongo.

Wakili: Umekua ukirudia mara kwa mara lini ilikuwa ya kwako?

Shahidi: Garri niliyonyang'anywa ni T 222 BDY V8 nilinunua 13/10/2020 toka kampuni ya Olicom 

Wakili: Bwana Sabaya umesema ulinunua hiyo gari ukwia na mke wako Jesca akiwa shahidi ushahidi wa manunuzi hayo uko wapi?

Shahidi: Mkataba wa gari hiyo kati ya Oilcom mimi upo Takukuru Jesca aliwapelekea maofisa wa Takukuru waliuomba, aliwapelekea kadi ya gari hilo hao Takukuru na gari hilo nilitoa milioni 35 na nikaongeza gari ingine ya awali wanaita ‘Kuvunja’ aina ya Prado ambayo namba ya usajili T 188 CJJ

Wakili: Unasema ulinunua gari Olicom na amekuja shahidi namba 12 Sabri Sharif anasema ilikua yake akakuuzia wewe na kuthibitisha hilo akaleta mkataba wa mauzo baina yake na wewe lakini wakati anahojiwa alisema hajawahi kuwa na umiliki wa gari hiyo wewe bwana Lengai unajiteteaje juu ya ushahidi wa sabri?

Shahidi: Kama hana nyaraka za gari aliuzaje gari? na alikiri uthibitisho wa gari ni kadi. Hata huu mkataba siufahamu 

Hakimu Kisinda aliahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo mshitakiwa huyo ataendelea kujitetea mahakamani hapo.

Advertisement