Sabaya,wenzake wawili wakutwa na kesi ya kujibu

Thursday August 12 2021
mahakamanipic

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya

By Mwandishi Wetu

Arusha. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu, Daniel Mbura, hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021.
Sabaya na wenzake wawili wanatuhumiwa kutenda makosa matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Sabaya na wenzake, wanatuhumiwa kutenda makosa hayo katika duka la Mohamed Saad huko eneo la Bondeni jijini Arusha, Februari 9 mwaka huu.

Soma zaidi:Mke wa diwani aangua kilio mahakamani akitoa ushahidi kesi ya Sabaya


Advertisement