Safari ya mwisho Sia na ndugu zake makaburini
Dar es Salaam. Miili ya watu watatu wa familia moja waliopoteza maisha kwa ajali ya gari usiku wa Agosti 02, mwaka huu; imepumzishwa katika makaburi ya Ununio kwa Kondo baada ya siku sita za maombolezo.
Miili hiyo iliyozikwa katika makaburi hayo, ni pamoja na ule wa Sia Msuya, Dk Norah Msuya na Diana Msuya ambao waliopoteza maisha wakiwa safarini kuelekea msibani wilayani Same, baada ya gari yao kugongana na Lori maeneo wialayani Chalinze.
Kabla ya shughuli ya kuzikwa milii hiyo, iliyoanza saa 11:46 jioni na kukamilika saa 12:30, kulitanguliwa na hafla fupi, iliyotoa fursa kwa ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wa kiserikali; kuaga katika viwanja vya gofu Kawe jijini Dar es Salaam.
Baada ya ibada fupi ya kuombea miili hiyo iliyofanyika kwa makanisa tofauti kulingana na imani za madhehebu ya marehemu hao, maziko makaburini hapo, yalihudhuriwa na watu mbalimbali.
Jeneza lilibeba mwili wa marehemu Sia ndiyo lilikuwa la kwanza kushushwa kwenye kaburi lake kabla ya kushusha lile lilibeba mwili wa Diana na baadaye lile lililobeba mwili wa Dk Norah.
Baada ya kushushwa baada ya kushushwa kwa majeneza hayo, familia ya wafiwa kwa maana ya Mzee Msuya, mkewe pamoja watoto wa marehemu hao, walianza kutia mchanga katika makaburi ya wapendwa wao hao, kabla ya kunikwa ikiwa ndiyo ishara ya hitimisho la maziko ya wanadugu hao.