Samaki wa Zambia waihangaisha TRA
Muktasari:
Kaimu Meneja wa TRA mkoani hapa, Davis Mongate alisema uchunguzi utavihusisha vyombo vyote vya dola.
Mbeya. Baada ya kukamatwa tani 27.5 za samaki wenye thamani ya Sh30.8 milioni waliokuwa wakisafirishwa kwenda Zambia, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani hapa imesema suala hilo linachunguzwa kwa umakini.
Kaimu Meneja wa TRA mkoani hapa, Davis Mongate alisema uchunguzi utavihusisha vyombo vyote vya dola.
Alisema wanatarajia kufanya kikao cha pamoja ili kupata taarifa za awali.
“Gari lile lilikuwa la ‘transit’ (kupita kwenda nje ya nchi), lakini limechepuka, wamefungua lakiri na kuondoa mtandao wa picha, wamepakua samaki ili wauzwe hapa wakati hawajulikani ubora wake hivyo yapo makosa mengi,” alisema.