Samia amteua Mwishawa kuongoza Tanapa
Massana Mwishawa aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Muktasari:
- Taarifa iliyotolewa leo, Julai 2, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imeeleza kuwa Mwishawa anachukua nafasi ya Mussa Kuji, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu katika nafasi hiyo.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Massana Mwishawa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Julai 2, 2026, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Mwishawa anachukua nafasi ya Mussa Kuji, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu katika nafasi hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi wa Mwishawa, unaanza kutekelezwa mara moja.
Tanapa ni taasisi ya umma iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye jukumu la kusimamia na kulinda hifadhi za taifa nchini na kuhifadhi wanyamapori, mimea na mifumo ya ikolojia.
Pia, Tanapa ina jukumu la kukuza na kusimamia utalii wa hifadhi za Taifa.
Kufanya utafiti na shughuli za uhifadhi wa mazingira na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maliasili.