Samia: Tanzania imejidhatiti kuingia katika masoko kimataifa kupitia kilimo

Muktasari:
- Tanzania imejidhatiti kuingia katika masoko ya kikanda na kimataifa kuuza mazao ili kukidhi mahitaji ya chakula katika nchi nbalimbali kwani inaamini inayo fursa ya kuwa mzalishaji na msafirishaji mkubwa wa mazao.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imejidhatiti kuingia katika masoko ya kikanda na kimataifa ili kukidhi mahitaji ya chakula katika nchi nbalimbali kwani anaamini kama nchi inayo fursa ya kuwa mzalishaji na msafirishaji mkubwa wa mazao.
Amesema anaamini bado upo wigo wa Tanzania kuwa wazalishaji wa mazao kama mahindi, mchele, mbogamboga na mafuta ya kula katika Jumuiya ya Afrika ya Mashari, nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika kwa ujumla.
Ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia marais waliohudhuria mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF), linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Samia amesema ili kuchochea kilimo biashara na kufikia malengo hayo, Tanzania sasa inatekeleza miradi ya kurahisisha usafiri na usafirishaji bidhaa kupitia nchi kavu, bahari na angani.
"Kuna miradi mikubwa ya kuzalisha nishati na kujenga kifumo ya mawasiliano ya haraka baharini ili kuwezesha kupatikana kwa maendeleo tarajiwa, yote haya yanalenga kurahisisha biashara kati ya Tanzania na nchi nyingine za afrika hususani kupitia soko Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA)," amesema Samia.
Amesema kupitia AfCFTA, tayari Tanzania imeanza utekelezaji kwa baadhi ya bidhaa zake kuuzwa katika nchi saba ambazo ni Cameroon, Misri, Ghana, Mouritiuos, Rwanda na Tunisia.
Kufuatia suala hilo amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika fursa za uwekezaji zinazolenga kuleta mageuzi katika kifumo ya chakula nchini.
"Matumaini yangu mkutano huu utakuja na mapendekezo yatakayoliwezesha bara kuwa na uendelevu wa kilimo na mifumo ya chakula, kubuni mikakati kuhusu lishe miongoni mwa nchi za Afrika na kufungua fursa za kilimo biashara na fedha," amesema Samia.
Alitumia rai hiyo kuzitaka sekta binafsi washirika wa maendeleo, AGRF, kuziunga mkono serikali za Afrika katika jitihada za kuendeleza sekta ya kilimo
"Hatua hizo ni muhimu katika kuimarisha mifumo ya chakula na kuhakikisha uendelevu wake. Katika muktadha huu natoa wito kwa Afrika kuonyesha mshikamano.