Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saratani ya damu, jicho yawatesa watoto nchini

Muktasari:

Saratani ya mtoto wa jicho na ile ya damu, imeelezwa kuwatesa zaidi watoto wadogo.

Dar es Salaam. Saratani ya mtoto wa jicho na ile ya damu, imeelezwa kuwatesa zaidi watoto wadogo.

Hayo yalisemwa jana na Mjumbe wa Bodi ya Asasi ya Tumaini la Maisha inayoshughulikia masuala ya kansa kwa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Gerald Mongella alipokuwa akipokea hundi ya Sh110 milioni iliyotolewa na Mo Dewji Foundation.

Mongella alisema ili kukabiliana na saratani hizo, wazazi hawana budi kuwafanyia vipimo vya uchunguzi watoto wao mara kwa mara.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano, Tanzania imefanikiwa kudhibiti ugonjwa huo kwa watoto kwa asilimia 50 hasa kwa wale wanaowahishwa hospitalini kwa matibabu.

“Kwa upande wa saratani ya mtoto wa jicho, tukigundua mapema, huwa tunachukua hatua ya kuliondoa ili isisambae,” alisema Dk Mongella.

Alisema takwimu zinaonyesha miaka ya nyuma hadi kufikia mwaka 2010, asilimia 10 tu ya watoto waliokuwa wakiugua maradhi hayo wakipatiwa matibabu walikuwa wakipona, lakini sasa ni asilimia 80.

Alitoa wito kwa wadau kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kutokomeza vifo vya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani.

Akizungumzia ugonjwa huo, Dk Janeth Kaijage alisema mwakani kutakuwa na kampeni maalumu kwa ajili ya kutoa elimu juu ya athari za ugonjwa huo na kuangalia njia bora za kuweza kupunguza kama sio kuutokomeza.

Alizitaja baadhi ya dalili za saratani kwa mtoto kuwa ni pamoja na sehemu ya shingo, shavu, tumbo au miguu kuvimba bila kuwa na maumivu, jicho la mtoto linabadilika na kuwa na wekundu, makengeza au upofu wa gafla, damu kutoka puani, kwenye fizi au kuvimba macho.