Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kuanza kulipa fidia KIA Agosti

Muktasari:

  • Baada ya tathmini kufanyika, Serikali inakusudia kutumia Sh11 bilioni kulipa fidia kwa wananchi wa vijiji vya Tindigani, Sanya stesheni na Chemka vilivyokuwa na mgogoro wa umiliki ardhi na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Hai. Baada ya tathmini kufanyika, mwezi Agosti mwaka huu, Serikali inakusudia kutumia Sh11 bilioni kulipa fidia kwa wananchi wa vijiji vya Tindigani, Sanya stesheni na Chemka vilivyokuwa na mgogoro wa umiliki ardhi na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Huku KIA ikiviona vijiji hivyo ambayo vinauzunguka uwanja huo, kama wavamizi wa eneo lake, lakini kwa upande mwingine, vijiji hivyo vilikuwa vinaiona KIA kama ndiye mvamizi wa maeneo yao, hali ambayo iliibua mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Katika kipindi chote hicho cha mgogoro, viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo mawaziri walifika katika eneo hilo kwa nyakati kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo bila mafanikio, hali iliyosababisha sintofahamu kati kampuni ya usimamizi na uendelezaji wa uwanja huo (KADCO) na wananchi wa vijiji hivyo.

Akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai, Mbunge wa jimbo hilo, Saashisha Mafuwe, amesema baada ya Serikali kukamilisha tathmini ya eneo lenye mgogoro katika uwanja huo wa ndege, wananchi hao wataanza kulipwa fidia za mali zao kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

"Tulikuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya uwanja wa ndege KIA wa kata tatu zinazozunguka uwanja wa ndege, habari njema ni kwamba baada ya Rais kushuka hapa tulikutana pale akatutaarifu yupo tayari na huenda baada ya mwezi huu wananchi wataanza kupata malipo ya fidia zao na mgogoro utakuwa umekwisha," amesema Saashisha

Saashisha amemshukuru Rais Samia kwa kuingilia kati mgogoro huo na kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia za mali zao.

"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendeleo huu mkubwa na wa pekee aliotupatia wananchi wa KIA, na kuhakikisha kwamba watu wanalipwa fidia ya mali zao," amesema mbuge huyo.

Naye, Mkuu wa Wilaya hiyo, Amiri Mkalipa amesema: “Rais wetu Samia Suluhu Hassan amekubali kuidhinisha Sh11 bilioni kwa ajili ya kuwalipa fidia watu ambao kimsingi walivamia eneo la uwanja wa ndege KIA, ambalo linamilikiwa na Serikali."

Kwa Mujibu wa DC huyo, licha ya wananchi hao kuvamia eneo hilo, Rais Samia ameona sio vizuri kuwaondoa bila kuwapa fidia itakayowasaidia kupata makazi mengine mapya na kuendeleza shughuli zao kama kawaida.

Aidha, Mkalipa amesema pamoja na Serikali kulipa fidia hizo, pia imetoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, ikiwemo Sh5.6 bilioni za ujenzi wa barabara, Sh3.4 bilioni za miradi ya maji na Sh3.4 bilioni kwa ajili ya ujenzi miundombinu elimu msingi na sekondari.