Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kuchukua hatua mwalimu aliyemrikodi mwanafunzi aliyekosea kusoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (aliyesmama) akifungua mafunzo kazini kwa walimu wa sekondari wa shule za Serikali na binafsi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wa masomo ya Kilimo na Sayansi kimu

Muktasari:

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amewataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarikodi wanafunzi ‘clip’ za video wanapokosea kusoma na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii.

Dodoma. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarikodi wanafunzi ‘clip’ za video wanapokosea kusoma na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii.

Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo baada ya clip ya video (bado haijajulikana ni shule gani) ambayo imekuwa ikisambaa katika mitandao ya jamii ikionyesha mwalimu akimrikodi mwanafunzi ambaye anakosea kusoma.

Kwa mujibu wa kitengo cha mawasiliano Serikali cha Wizara hiyo, Profesa Mkenda ametoa wito huo leo Jumatano Mei 4, 2022 mkoani Morogoro alipokuwa akifungua mafunzo kazini kwa walimu wa sekondari wa shule za Serikali na binafsi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wa masomo ya Kilimo na Sayansi kimu.

Amesema vitendo hivyo ni kinyume na maadili ya walimu kwasababu katika mchakato wa kujifunza wanafunzi wana faragha ambazo zinapaswa kulindwa na walimu hao.

“Kwa mfano unakuta kuna clip chache zinazunguka unakuta mwalimu anamhoji mwanafunzi halafu anatape (anarikodi) halafu inazunguka hao tutashirikiana kuwashughulikia,”amesema.

Amewataka walimu nchini kutoharibu taswira njema ya walimu kwasababu wanapopiga picha hizo na kuzisambaza wazazi wanadhani kuwa walimu wote ndio walivyo kumbe sivyo.

 "Tunakemea walimu wote wenye tabia ya kuwarekodi wanafunzi na kusambaza katika mitandao ya kijamii na wale watakaopatikana kutenda kosa hilo watachukuliwa hatua za kinuhamu kwani hii ni kuigilia faragha ya mwanafunzi katika kujifunza," amesema.

Profesa Mkenda amesema kazi ya ualimu ni wito kwa kuwa ni ya kufundisha na kulea vijana, hivyo ni muhimu kwa walimu kutambua wana dhamana kubwa ya kuwalea vijana ili wawe na nidhamu na maadili.

Kuhusu mafunzo ya walimu kazini, Profesa Mkenda amesema mafunzo hayo yatakuwa endelevu na kwamba katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 wizara imetenga Sh1.2 bilioni kwa ajili ya mafunzo hayo.

"Kwa muda mrefu walimu wamekuwa watu wa kubaki darasani na chaki huku wenzao wanakwenda katika semina, warsha na makongamano sasa ni wakati wao wa kupata mafinzo kazini ambayo yatawawezesha kupata mbinu za kufundushia kutokana na mabadiliko yanayoendelea duniani,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Aneth Komba amesema Serikali imeipatia fedha TET kwa ajili ya kutoa mafunzo kazini kwa walimu.