Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 12,476 sekta ya afya

Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 12,476 sekta ya afya

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema sekta ya afya katika mwaka wa fedha 2020/21 itaajiri watumishi wapya 12,476.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema sekta ya afya katika mwaka wa fedha 2020/21 itaajiri watumishi wapya 12,476.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Februari 10, 2021 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dk Godwin Mollel wakati akijibu mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mwantum Zodo.

“Sekta ya afya nchini ina upungufu wa watumishi 16,000, Serikali in mpango gani katika kukabiliana na changamoto hiyo,” amehoji mbunge huyo.

Katika majibu yake, Dk Mollel amesema upungufu wa watumishi katika sekta ya afya umetokana na mahitaji mapya yanayotokana na upanuzi wa hospitali za kanda, ujenzi na upanuzi wa hospitali za rufaa za mikoa 10, kukamilika kwa ujenzi wa hospitali za halmashauri 102, kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya afya 487 na zahanati 1,198.

Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi na katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2020 Serikali imeajiri watumishi 14,000.

Dk Mollel amesema zaidi ya watumishi 565 walipatiwa ajira za mikataba kwa kugharamiwa na makusanyo ya vituo vya kutolea huduma na wengine kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Amebainisha kuwa Serikali imeendelea kutoa ajira mbadala ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliostaafu, kuacha kazi au kufariki.

Amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 sekta ya afya inatarajia kuajiri watumishi wapya 12,476.