Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaja na mbinu mpya usimamizi mikopo asilimia 10

Serikali yaja na mbinu mpya usimamizi mikopo asilimia 10

Dododma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amesema Serikali itaimarisha usimamzi wa utaoji wa mikopo ya asilimia 10 kwenye halmashauri kwa kutumia mifumo ya Tehama ili mikopo hiyo iweze kuwanufaisha wahusika na kuleta mabadiliko chanya kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Waziri Bashungwa ameeleza hayo leo Ijumaa Juni 24, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu  ya  Serikali ya mwaka wa fedha 2022/23 na kueleza kuwa mfumo wa kielektroniki utasaidia kuongeza usimamizi kwa kutambua anayepewa mkopo, shughulli anayoifanya na urejeshaji wa mkopo katika halmashauri zote nchini.

“Tutasimamia Sheria za utoaji wa mikopo ya asilimia 10 na kuhakikiha kila Mkurugenzi anatoa mikopo hiyo kwa wakati na sio kwa hiari bali ni takwa la sheria na kuzingatia utawala bora katika usimamizi wa mikopo hiyo” amesema Bahungwa.

Bashungwa amesema moja ya kigezo kitakachotumika kupima ufanisi  wa wakurugenzi katika halmashauri ni usimamizi wa utoaji na urejeshaji wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Amesema Serikali itaimarisha nidhamu katika Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa na kuhakikisha wakuu wa mikoa, wilaya na wakurungenzi wa Halmashauri wanatoa ushirikiano kwa wabunge ambao ni watetezi na wawakilishi wa wanannchi.

Amesema  Tamisemi inaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya halmashauri na kuzipati ufumbuzi wa haraka lengo likiwa ni kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi