Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yajitwisha kero za mabaharia Tanzania

Muktasari:

  • Mabaharia wa Tanzania wamebainisha changamoto zinazowaoabili huku Serikali ikiahidi kwenda kuzifanyia kazi

Bagamoyo. Serikali ya Tanzania imesema itazifanyia kazi changamoto na fursa zinazowakabili mabaharia nchini.

Miongoni mwa changamoto hizo ni nyenzo dhaifu za kusimamia mambo ya bahari yaani mbinu zisizo za wazi na zenye kuakisi wakati uliopo.

Ukosefu wa sera na kanuni za ajira za ubaharia na kuwepo kwa mifumo kandamizi za uwajiri wa mabaharia hususan katika kampuni za ndani.

Nyingine ni stahiki duni za mabaharia kama fidia, bima, hifadhi ya jamii, mafunzo kwa vitendo, mazingira mabovu ya kazi kwa mabaharia na hali zao za kimaisha hususan kwa vijana na wanawake.

Changamoto hizo zimebainishwa na Chama cha Mabaharia Tanzania (Tasu) na Zanzibar (Zasu) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya  Mabaharia duniani, leo Jumanne, Juni 25, 2024.

Tanzania yamefanyika Uwanja wa Njianjema, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Uchaguzi, David Kihenzile. Kauli mbiu kwa mwaka huu ni “Mustakabali wa uendeshaji vyombo vya usafiri majini.”

Akisoma risala ya mabaharia, Katibu wa Vijana wa Tasu na Zasu, Ally Mzee amesema edapo mambo kadhaa ya kimkakati yakifanyika kwa juhudi za makusudi ikiwamo tafiti na kaguzi mbalimbali za kina zinaweza kuibua fursa.

Amezitaja fursa hizo ni kutambua idadi kamili ya mabaharia waliopo Tanzania na kujiunga na vyama vya wafanyakazi, kutambua idadi kamili ya kampuni za meli zinazoendesha shughuli zake Tanzania yote.

Pia, kutambua mabaharia na uwezo wao, kupata utambulisho mzuri wa vyama kitaifa na kimataifa, kutumika kwa kazi za kando ya bahari na ajira za mabaharia katika meli za kigeni hususan zenye usajili wa bendera ya Tanzania.

"Baharia anapitia changamoto nyingi, mazingira mabovu ya kazi kwa sababu tunateseka. Nahodha anaendesha chombo analipwa laki mbili, anarudi nyumbani hana kitu na kuonekana msela, tunaomba Serikali ifanyie kazi maombi yetu," amesema Mzee.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa taasisi, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dk Tumaini Gurumo,"mabaharia wanafanya kazi kubwa sana lakini wako nyuma ya pazia. Tunashangilia bandari zinaingiza mzigo mkubwa, fedha zinaongezeka lakini haya ni matunda ya mabaharia."

Akifunga maadhimisho hayo yaliyoanza Juni 22, Naibu Waziri Kihenzile amesema asilimia zaidi ya 80 ya shehena duniani inasafirishwa na mabaharia hivyo ni eneo muhimu.

"Tumeyapokea. Tutakwenda kuyafanyia kazi hatua kwa hatua yale yote mliyotueleza.

Ametoa wito kwa wananchi na mabaharia kuzingatia taarifa za hali ya hewa zinapotolewa ili kuepuka madhara yanayoepukika ikiwamo vyombo kupotea njia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac), Mohamed Salum amesema siku ya leo inatumika kutafakari mchango mkubwa wa mabaharia duniani.

Salum amesema baadhi ya changamoto zilizoelezwa wamekwishaanza kuzifanyia kazi ikiwamo hilo la ajira kwa kuandaa makubaliano ya ushirikiano na nchi 16 ambazo zikifanikiwa itakuwa faraja kwa mabaharia.