Serikali yakusanya kodi Sh1.9 trilioni Septemba

Saturday October 02 2021
By Mwandishi Wetu

Morogoro. Serikali imesema imekusanya kodi ya Sh1.9 trilioni kwa kipindi cha Septemba mwaka huu ikiwa ni sawa na asilimia 93.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumamosi, Oktoba 2, 2021 Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema makusanyo hayo ni makubwa kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2020.

Soma zaidi:Kamati bei ya mafuta yakabidhi ripoti kwa Waziri Mkuu

“Tuliweka malengo ya kukusanya Sh2.1trilioni, ukusanyaji huu ni mkubwa ukilinganisha na mwaka jana kipindi kama hiki tulikusanya Sh1.7 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 80 ya malengo tuliyojiwekea ya kukusanya Sh2.2 trilioni” amesema Msigwa.

Advertisement