Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yapiga ‘stop’ ujenzi eneo la Uhuru Park Moshi

New Content Item (1)

Eneo la Uhuru Park ambako ujenzi ulikuwa unaendelea Manispaa ya Moshi.

Muktasari:

  • Hivi karibuni, Mbunge wa Moshi mjini (CCM), Ibrahim Shayo akiwa bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, aliibua hoja kuhusu madai ya kubadilishwa kwa matumizi ya baadhi ya maeneo ya wazi ndani ya Manispaa hiyo, akitaka kujua hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi wanaokiuka taratibu za matumizi ya ardhi.

Moshi. Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro imesimamisha kwa muda ujenzi unaoendelea katika eneo la wazi la Uhuru Park, Manispaa ya Moshi, baada ya kubaini kuwa taratibu za kuomba kibali kutoka Wizara ya Ardhi hazikufuatwa. Hatua hiyo imekuja  siku chache baada ya Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba kuagiza uchunguzi wa suala hilo.

Akizungumza leo Alhamisi, Julai 16, 2026, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa amesema uamuzi huo umetokana na maelekezo ya Kamati ya Usalama ya Mkoa, ambayo imetekeleza agizo la Waziri Mkuu kwa kufanya uchunguzi na kubaini hali halisi ya suala hilo.

Nzowa amesema kabla ya kuanza shughuli yoyote ya maendeleo katika eneo la wazi, ni lazima mwendelezaji aombe na apate kibali kutoka wizara yenye dhamana ya ardhi kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi.

Amesisitiza kuwa katika ujenzi unaoendelea katika eneo la Uhuru Park, taratibu hizo hazikufuatwa, hali iliyosababisha Serikali ya Mkoa kuagiza shughuli zote za ujenzi kusimamishwa kwa muda hadi taratibu nyingine  zitakapokamilika.

Katibu tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa akizungumza ofisini kwake leo Julai 16, 2026 kuhusu kusimamishwa kwa ujenzi katika eneo la Uhuru Park. Picha na Janeth Joseph

"Sisi kama mkoa tumetimiza wajibu wetu, kwasababu yalikuwa ni maelekezo ya Waziri Mkuu, kufuatilia tuone hali ilivyo na tuchukue hatua. Mkoa tumefuatilia na kamati ya usalama ya mkoa, tumekwenda kwenye lile eneo tukapata maelezo ya mkurugenzi tangu ujenzi ulivyoanza na utaratibu uliotumika,"amesema Nzowa .

"Tulimshirikisha kamishana  Msaidizi wa ardhi  wa mkoa wa Kilimanjaro. Hivyo tumeona uhalisia wa lile eneo lakini kwa maelezo ya kamishna, kuna taratibu fulani katika lile eneo hazikufuatwa, kwamba  unapotaka kuendeleza eneo ambalo ni la wazi, kibali kinapaswa kuombwa na kutolewa na wizara ya ardhi,” amesema.

Aidha, amesema kufuatia hali hiyo,  tayari taratibu zimeshaanza kushughulikiwa za kuomba kibali kuendelea na ujenzi uhuo kutoka Wizara ya ujenzi.

"Ofisi ya Mkurugenzi iliandika barua hapa kuomba hicho kibali na sisi tumeshaandika na kumepelekwa wizarani kwa hiyo tunasubiri majibu ya wizara," amesema Nzowa

Hivi karibuni, Mbunge wa Moshi mjini (CCM), Ibrahim Shayo akiwa bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, aliibua hoja kuhusu madai ya kubadilishwa kwa matumizi ya baadhi ya maeneo ya wazi ndani ya manispaa hiyo,  akitaka kujua hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi wanaokiuka taratibu za matumizi ya ardhi.

Eneo la Uhuru Park ambako ujenzi ulikuwa unaendelea Manispaa ya Moshi.

Mbunge huyo aliiomba Serikali kutoa kauli kuhusu madai ya ukiukwaji wa matumizi ya eneo hilo kubadilishwa matumizi.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu, pale Moshi Mjini kuna eneo la wazi katikati ya mji linaitwa Uhuru Park. Eneo hilo lina zaidi ya miaka 50, lakini leo baadhi ya viongozi wameanza kujenga pale. Wanajenga vibanda vya biashara kama vile vinavyozunguka masoko ya katikati ya miji, jambo ambalo si zuri. Wananchi wengi wanamiminika katika ofisi ya mbunge wakilalamikia hali hiyo," alisema Shayo.

Akijibu hoja hiyo, Mwigulu aliiagiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kufuatilia na kuangalia madai hayo na kama yapo yafuate utaratibu.

Mpaka sasa ujenzi katika eneo hilo umesimama kusubiri majibu kutoka Wizara ya Ardhi.