Serikali yasitisha ukaguzi EFD kwa wafanyabiashara Kariakoo

Dodoma. Serikali imesitisha kazi ya ukaguzi wa risiti za kielektroniki (EFD) na ritani za kodi  iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, jijini  Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 24, 2024 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo kwa niaba ya Serikali wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya viongozi wa wafanyabiashara Tanzania, viongozi wa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara.

Kikao hicho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.


Endelea kufuatilia mitandao yetu