Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yataka kesi ya kupinga ving’amuzi kuondoa chaneli za ndani itupwe

Muktasari:

Mahakama kuamua kama kuna kesi ya kujibu au la Septemba 10


Iringa. Mwanasheria wa Serikali, Mwinyiheri Aristaric ameiomba mahakama kutupilia mbali maombi ya kutaka kubatilishwa kwa amri ya kuondolewa chaneli za ndani kwenye ving’amuzi vya baadhi ya kampuni yaliyokuwa yanatoa huduma ya kurusha maudhui yanayorushwa na chaneli za ndani.

Mwinyiheri ameeleza hayo leo Septemba 4,2018 katika Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kwamba waleta maombi wameshindwa kuainisha ni kipengele gani cha sheria kilichowaongoza kupeleka maombi hayo.

Amesema maombi yalipaswa kuletwa kwa kutumia kifungu cha 19(2)(3) cha sheria inayopatikana katika sura ya 310 (Law reform (fatal accidents) miscellaneous provisions Act).

Amesema sheria inaitaka mahakama kusikiliza maombi hayo ndani ya siku 14 na  Mahakama imeshindwa kusikiliza maombi hayo kutokana na baadhi ya wajibu maombi kutokuwepo mahakamani baada ya waleta maombi kushindwa kuwafikishia samansi za mahakama kwa wakati.

Akijibu hoja hizo, wakili upande wa waleta maombi, Edmund Mkwata amesema Mahakama haifungwi na sheria kutosikiliza maombi hayo katika hatua za awali kwa sababu baadhi ya wajibu maombi kutowepo mahakamani badala yake sheria inahitaji wajibu maombi wawepo kama Mahakama itaona kuna uhitaji wa wao kuwepo.

Baada ya kusikiliza uwasilishaji huo kutoka pande zote mbili, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Penterine Kente aliahirisha shauri hilo mpaka Septemba 10, 2018  atakapotoa uamuzi wa ama mahakama kusikiliza maombi hayo au kutupilia mbali.

Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2018 waleta maombi Silvanus Kigomba, Jesca Msambatavangu, Oliver Motto, Emmanuel Sebastian Atilio na Hamdun Abdallah wameiomba Mahakama Kuu kubatilisha amri ya kuondolewa chaneli za ndani kwenye ving’amuzi vya Azam, Dstv, Zuku na Star Times ili kutoa nafuu kwa watumiaji wa vingamuzi hivyo kuendelea kupata matangazo ya chaneli za ndani kupitia.