Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatoa mikopo ya Sh1.2 bilioni kwa wafanyabiashara Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude (katikati, mwenye suti ya bluu), akikabidhi hundi yenye thamani ya Sh1.2 bilioni kwa vikundi 101 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuimarisha mitaji ya shughuli zao za kiuchumi, jijini Arusha.

Muktasari:

  • Mikopo hiyo imetolewa leo Juni 6, 2026 kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Arusha. Halmashauri ya Jiji la Arusha imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Sh1.211 bilioni kwa vikundi 101 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Mikopo hiyo imetolewa leo Juni 6, 2026 kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Akikabidhi hundi za mikopo hiyo kwa wanufaika, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, amesema mikopo hiyo inalenga kuwezesha makundi hayo kuanzisha, kuendeleza na kupanua shughuli za kiuchumi zitakazoongeza kipato na kuboresha maisha yao.

Amesema kuwa baadhi ya waombaji hukosa nafasi kutokana na kukosa nidhamu, uvumilivu na ufuatiliaji wa mahitaji muhimu ya mpango huo, ikiwemo kutimiza masharti muhimu.

Mkude aliwataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili ziweze kuleta matokeo chanya katika biashara na miradi yao ya uzalishaji mali.

Pia aliwahimiza kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuifanya programu hiyo kuwa endelevu na kuwezesha vikundi vingine kunufaika katika awamu zijazo.

Meya wa Jiji la Arusha, Maxmillian Iranghe, amesema utoaji wa mikopo hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi wanapata mitaji na fursa za kiuchumi zinazowawezesha kujitegemea na kuinua hali zao za maisha.

"Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa mpango wa mikopo ya asilimia 10 kwa lengo la kuwajengea uwezo wananchi na kuchochea maendeleo ya uchumi katika ngazi za jamii."

Mmoja wa wanufaika wa mkopo huo, Elijah Hashim, amesema kuwa kikundi chake kimepata mkopo huo baada ya kuomba kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

"Masharti mengi yalikuwa ni kutambuana katika biashara, barua za utambuzi na pia namna ya kurejesha, ambapo vyote tulijaza na kuwasilisha, na leo tumefanikiwa kukabidhiwa hundi ya Sh12 milioni," amesema.