Serikali yatoa Sh10.9 bilioni fedha za miradi ya maendeleo Buchosa

Thursday November 25 2021
shigongopic
By Daniel Makaka.

Buchosa. Serikali imetoa Sh10.9 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo Alhamisi Novemba 25, 2021 mbunge wa jimbo hilo, Eric Shigongo amesema kati ya fedha hizo Sh2.4 bilioni ni kwa ajili ya barabara, Sh2.5 bilioni kwa ajili ya elimu, Sh1 bilioni zitatumika katika ujenzi wa vituo vya afya kata ya Maisome na Kata ya Nyanzenda.

Amesema Sh5 bilioni zitatumika kusambaza mtandao wa maji katika jimbo hilo.

Wakati huo huo, Shigongo amesema kuwa Serikali imetenga Sh82 bilioni za kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 68.

Advertisement