Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yazungumzia malipo ya wananchi ambao mazao yao yameharibiwa na tembo

Serikali yazungumzia malipo ya wananchi ambao mazao yao yameharibiwa na tembo

Muktasari:

  • Serikali imesema shughuli ya kulipa fidia wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa na tembo nchini inaendelea.

Same. Serikali imesema shughuli ya kulipa fidia wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa na tembo nchini inaendelea.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Mei 23, 2021  na naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Marry Masanja wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Maore Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

"Ni kweli changamoto hii ya tembo ipo na ndio maana Serikali inasimamia kwa umakini mkubwa kuhakikisha tunapoendeleza utalii hatuwabudhiwi  wananchi, hivyo fidia za wananchi walioathiriwa na tembo zinaendelea kulipwa maeneo mengi nchini na wale ambao hawajalipwa watalipwa fedha zao," alisema Masanja.

Amesema ili kuepuka mwingiliano wa wanayama na wananchi Serikali imeandaa utaratibu wa kuchimba mabwawa kwenye maeneo ya hifadhi na maeneo ya wananchi.

"Namwagiza katibu mkuu wa wizara kuhakikisha yanachimbwa mabwawa ndani ya hifadhi na wananchi wanachimbiwa mabwawa yao ili mwingiliano wa wananchi na wanyama usiwepo na zoezi hili lifanyike mara moja ili wananchi waishi kwa amani," amesisitiza,

Awali akitoa taarifa kwa naibu waziri, mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi, Emmanuel Mwairano amesema  kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi 2020 km Wilaya ya Mwanga na Same jumla ya ekari 5873 ziliharibiwa na tembo, vifo vya mifugo 98 vilitokea,  vifo vinne vya binadamu na majeruhi 11.