Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh3.1 bilioni zatolewa ununuzi mabehewa 1,430 ya SGR

Muktasari:

Wakati Shirika la Reli (TRC) likisaini mkataba wa ununuzi wa mabehewa ya mizigo 1,430 kwa ajili ya treni ya kisasa SGR, Serikali imetoa Sh3 bilioni kwa ajili ya kununua mabehewa hayo.

Dar es Salaam. Wakati Shirika la Reli (TRC) likisaini mkataba wa ununuzi wa mabehewa ya mizigo 1,430 kwa ajili ya treni ya kisasa SGR, Serikali imetoa Sh3 bilioni kwa ajili ya kununua mabehewa hayo.

Hayo yamesemwa leo Februari 8, 2022 na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati TRC ikisaini mkataba huo wenye thamani ya Dola za Marekani 127.2 milioni na kampuni ya CRRC International ya nchini China ambao ni watengenezaji wa mabehewa hayo.

“Serikali ya Rais Samia imetoa Sh3.1 bilioni kwa ajili ya mradi huu wa ununuzi wa mebehewa haya ya treni iendayo kasi. Nasi tunaamini kwamba wasimamizi mtafanya kazi yenu vizuri ili thamani ya hii fedha ionekane,” amesema.

Profesa Mbarawa amesema uwepo mabehewa hayo utawezesha ubebaji wa tani 10,000 kwa treni moja sawa na maroli 500 barabarani.

“Behewa hizi zipo 60 za kubebea mifugo ambapo moja linauwezo wa kubeba ng’ombe 100 hivyo itaweza kubeba ngombe 6000 kwa wakati mmoja...

“Magari behewa moja linaweza kubeba magari nane hivyo kwa treni moja lenye behewa 50 litaweza kubeba magari 400 hii itasaidia kupunguza ajali za barabarani kwani mizigo itasafirishwa kwa treni itafika kwa wakati na kwa gharama nafuu,” amesema Profesa Mbarawa.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema mkataba huo ni wa miezi 12 utakaohusisha usanifu na utengenezaji wa behewa kwa ajili ya kubeba mizigo ya aina mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya mteja kupitia reli ya kisasa.