Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku 30 za Simbachawene kuhusu silaha

Siku 30 za Simbachawene kuhusu silaha

Muktasari:

  • Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene ametoa siku 30 za kusalimisha silaha haramu kwa hiari nchi nzima.



Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene ametoa siku 30 za kusalimisha silaha haramu kwa hiari nchi nzima.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 30, 2021, Simbachawene amesema shughuli hiyo ya kusalimisha silaha itaanza Novemba Mosi hadi Novemba 30,  2021.

“Kupitia tangazo la Serikali namba 774 la  Oktoba 29, mwaka huu natangaza msamaha wa kutoshtakiwa kwa wale watakaosalimisha silaha kwa hiari kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye tangazo,” amesema Simbachawene.

Amesema silaha hizo zisalimishwe katika vituo vyote vya jeshi hilo nchini na ofisi za Serikali za mitaa na kwa watendaji wa kata kuanzia saa mbili  asubuhi hadi saa 10 jioni.