Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wavamia vijiji, waua ng’ombe wanne

Wananchi wa kata ya Maboga wakimueleza Diwani  hali halisi ya usalama katika kijiji chao.

Muktasari:

  • Hofu imetanda kwa wakazi wa Magunga na Ihami katika Kata ya Maboga, Iringa baada ya kundi la simba kuvamia vijiji hivyo kwa nyakati tofauti na kuua ng'ombe wanne.


Iringa. Hofu imetanda kwa wakazi wa Magunga na Ihami katika Kata ya Maboga, Iringa baada ya kundi la simba kuvamia vijiji hivyo kwa nyakati tofauti na kuua ng'ombe wanne.

Taarifa kutoka Maboga zinaeleza kuwa kuwa simba hao waliianza kuvamia Kijiji cha Magunga kabla ya kwenda Ihami ambako walivamia zizi na kuwaua ng’ombe hao wane.

Akizungumzia tukio hilo, mfugaji Felix Malekela anasema alisikia vurugu ndani ya zizi na alipofuatilia aliona kundi kubwa la samba.

“Ndipo nilipoanza kupiga kelele nikisaidiana na majirani hali iliyowafanya wakimbie japo tayari ng’ombe walikuwa wameshaliwa.

Taarifa kutoka Ihami zinaeleza kuwa wanavijiji na askari wa wanyamapori wameungana kuwasaka wanyama hao.

Nae bibi Mgovano ambaye ng'ombe zake zimeliwa na simba hao amesema alisikia mbwa zinabweka huku zinakimbia hivyo alihisi kuna shida lakini kutokana na umri wake wa uzee alishindwa kufanya lolote.

Bibi Mgovano amesema kulivokucha asubuhi hakukuta ng'ombe na baada ya kupiga kelele majirani walipofika ndipo kufanya utafiti na kugundua kuna miguu ya simba ndiyo iliyopita.

Bibi huyo anayeishi peke amesema anaamini simba hao ni wanyama tu na anaiomba serikali wamfikirie siku hizi mbili tatu kwani ng'ombe hao ndio walikuwa tegemeo la kila kitu kwake.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Maboga Venserus Muyinga amesema tukio hilo ni la pili lilitokea, mwaka 1981 katika kata kuliwahi kutokea tukio la ng’ombe kuliwa na wanyama mwitu hata hivyo hili la kuvamiwa na simba halikuwahi kutokea.

Muyinga amesema katika tukio hilo lilivotokea alichukua hatua ya kupiga simu kwa watu wanaohusika na wanyama  na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa na kupatiwa msaada wa vikosi viwili askali wa maliasili ambavyo bado vinafanya kazi kuwasaka simba hao.

Muyinga ameendelea kuwaomba wanakijiji wenzake kuwa macho na wageni hao hatari kwani wanahatarisha maisha ya binadamu na mifugo pia.

"Jamani tutulie huyu mgeni wetu ni mkali hakuna asiyefahamu, na leo wanaweza kuwa kijiji hiki kesho kijiji kingine," alisema Muyinga

Nae balozi wa kijiji hicho cha Ihami Speransia Dalu amewaomba wananchi kutotembea hovyo hovyo kutokana na hali inayoendelea katika kata hiyo.