Simbakalia mwenyekiti mpya bodi ya NARCO
Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia Mwenyekiti Mpya wa Bodi Tendaji ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).
Muktasari:
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Kanali mstaafu Joseph Simbakalia kuwa Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).
Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Kanali mstaafu Joseph Simbakalia kuwa Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu leo Septemba 3, 2023.
Kanali Simbakalia anachukua nafasi ya Mhandisi Cyprian Luhemeja aliyeteuliwa kuwa katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu)
Simbakalia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji, wa Mauzo ya Nje Tanzania (EPZA).
Narco ni kampuni iliyochini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa na jukumu la ufugaji na uzalishaji wa mifugo na bidhaa za mifugo pamoja na kuendeleza ranchi. Vilevile kununua mifugo kutoka kwa wafugaji wa asili kwa ajili ya kuwanenepesha na kuuza.