Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SMZ, LSF wazindua wiki ya msaada wa kisheria

Ofisa Programu Mwandamizi kutoka Ofisi za Legal Services Facility (LSF) Visiwani Zanzibar, Alphonce Gura akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar mwaka 2023.

Muktasari:

  • Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar 2023 yamezinduliwa na Waziri, Haroun Ali Suleiman, ambapo shughuli mbalimbali za kutoa elimu na msaada wa kisheria zitafanyika na yatahirimishwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi Julai 22.

Dar es Salaam. Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kupitia Idara ya Msaada wa Kisheria Zanzibar kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF) wamezindua maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria visiwani humo kwa mwaka 2023 kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na kuwafikia wananchi wenye uhitaji wa huduma hiyo.

 Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar yanafanyika huku yakipambwa na shughuli mbalimbali za kijamii lengo likiwa na kuhamasisha jamii kufikiwa na huduma za msaada wa kisheria popote zilizo bila kikwazo. 

Taarifa iliyotolewa na LSF leo Jumanne, Julai 18, 2023 imesema miongoni mwa shughuli zitakazofanyika katika wiki hii ni pamoja na utoaji wa elimu ya kisheria kupitia vyombo vya habari na uendeshaji wa jukwaa la kona ya msaada wa kisheria ili kuyafikia makundi yote katika jamii.

Nyingine ni pamoja na kutembelea makundi yaliyoko vizuizini (magerezani/rumande au vyuo vya mfunzo) pamoja uandaaji wa bonanza la msaada wa kisheria kwaajili ya kupaza sauti kuhusu kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji katika jamii.

Waziri Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar mwaka 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho haya Zanzibar, Waziri Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman amesema kuwa maadhimisho hayo ni hatua ya serikali kuwajali wananchi wake.

“Shughuli ni muhimu kwakuwa tunalenga kuhakikisha kuwa Zanzibar inazungukwa na jamii yenye ustawi mzuri uliomarika katika kila nyanja ya maisha pamoja na kuhakikisha wananchi wake hususani wanyonge na wasiojiweza wanapatiwa msaada wa kisheria bila ya usumbufu wowote.

"Lengo kuu la Wiki ya Msaada wa Kisheria ni kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa jamii yetu inayotuzunguka,” amesema Waziri Suleiman.

Kwa upande wake, Ofisa Programu Mwandamizi kutoka LSF visiwani humo, Alphonce Gura amesema kuwa shirika hilo ni mdau mkuu katika maadhimisho hayo kwa kuwa tukio hilo linalenga kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi ili kuongeza upatikanaji wa haki bila kikwazo chochote kile.

“LSF kazi yetu kubwa ni kukuza upatikanaji wa haki kupitia uwezeshaji wa kisheria kwa wananchi wote hususani wanawake na wasichana. Hivyo kupitia maadhimisho haya tutaweza kuwafikia watu wote kupitia shughuli mbalimbali ambazo zinakwenda kufanyika katika kipindi hiki cha maadhimisho,” amesema Gura.