Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Songwe kutumia afua za mpango kupambana na maambukizi ya VVU

Mkurugenzi wa Idara ya Jamii kutoka Shirika la HJFMRI ,Hija Wazee akizungumza na wadau sekta ya afya watendaji wa kata na mabinti wanaonufaika na mradi wa  kusaidia mabinti wanaoishi katika mazingira magumu. Picha na Hawa Mathias

Songwe. Mkoa wa Songwe umezindua utekelezaji wa afua zilizo chini ya mpango wa Determined, Resilient, Empowered, AIDS-free, Mentored and Safe (DREAMS) zinatotekelezwa na Shirika la HJFMRI  ikiwa ni njia mahususi ya kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) katika mpaka wa Tunduma kwa wasichana rika balehe na wanawake vijana.
Mpango huo ambao umeanza kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe kutokana na  kukidhi vigezo kulingana na hali ya  maambukizi kuwa juu  kwa  asilimia 5.8 zaidi ya malengo ya kitaifa ya asilimia 4.7 ni mpango mahususi unaolenga kupunguza maambukizi ya VVU kwa mabinti balehe na wanawake vijana wenye umri wa miaka 15 – 24.
Kupitia mpango huu, wanufaika wa mradi ni mabinti walio kwenye mazingira hatarishi ikiwemo waliozaa kwenye umri mdogo, wanaoishi na maambukizi ya VVU, wenye mahusiano na mpenzi zaidi ya mmoja, walioolewa katika umri mdogo, mabinti waliocha shule, na mabinti wanaongoza kaya katika jamii.
Hijja Wazee, Mkurugenzi wa Idara ya Jamii kutoka Shirika la HJFMRI, amesema mradi huo unafanya vizuri katika Halmashauri ya Mbeya Mjini, Mbarali na Kyela ambapo mabinti wameweza kujikwamua kiuchumi na kuelimisha vijana wenzao kujikinga na maambukizi ya VVU.
Awali, akielezea lengo la mpango wa DREAMS na matarajio, Mtendaji wa Mradi wa Nyada za Juu Kusini unaotekelezwa na  Dhirika la la HJFMRI, David Maganga amesema kuwa kupitia mradi huo wanatarajia utaleta chachu ya mabadiliko na kupunguza maambukizi ya Ukimwi katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Amesema kuna wadau mbalimbali hususan Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Ukimwi (PEPFAR) kupitia Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) ya Idara ya Ulinzi ya Marekani (US. DoD) wamekuwa na mchango mkubwa kwa Serikali katika kufanikisha mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi kwa kufadhili Shirika la HJFMRI litekeleze afua hizi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na hivyo ni matarajio yao mradi huo utafanya vizuri pasipo udanganyifu.
Mratibu wa Tume ya Kupambana na Ukimwi (Tacaids)  Mkoa wa Songwe , Emmanuel Petro amesema kutokana na hali ya maambukizi kuwa juu kwa asilimia 5.8 na mwingiliano wa watu kutoka sehemu mbalimbali, halmashauri  hiyo imekidhi vigezo vya kufikishiwa mradi ya DREAMS.
Petro ametaja sababu za  Mkoa wa Songwe kuwa juu katika maambukizi ni kutokana na mwingiliano wa shughuli za kiuchumi hususan madereva wa mizigo kukaa kwa muda mrefu mpakani na hivyo kujiingiza kwenye mahusiano ya kufanya ngono zisizo salama na kusababisha hali kuwa mbaya ya maambukizi.
“Kwa  takwimu za mwaka 2017 zinaonyesha asilimia 80 ya vijana nchini wamepata maambukizi hali ambayo inapunguza nguvu kazi kwa taifa hivyo kuna kila sababu wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kukabiliana na janga hilo,”amesema.
 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Dk Enock Mwambalaswa amesema kuwa ujio wa mradi huo utasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya Ukimwi kwa vijana kupitia elimu na uhamasishaji.
”Tunashukuru ujio wa mradi huu kama mnavyojua mji wa Tunduma umechangamka kwa shughuli za kibiashara na mwingiliano wa watu kutoka mataifa mbalimbali hivyo kuwepo kwa mahusiano mengi ya kingono,”amesema.
Mnufaika kupitia Mradi wa Dreams, Leonia Sungura amesema  awali kabla ya kutambulika alikuwa akiishi katika mazingira magumu ambapo kwa sasa amejitambua na kuwa balozi wa kutoa elimu kwa mabinti rika balehe kujikinga na maambukizi kwa kuepuka ngono zisizo salama.
“Tunaomba Serikali kuendelea kushirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya VVU kwani kundi kubwa tunaoathirika ni vijana ambao ni nguvu kazi kwa taifa na kinachochangia kujiingiza kwenye ngono zisizo salama ni hali duni ya maisha miongoni mwetu,” amesema.