Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Songwe yavuka lengo chanjo ya polio

Muktasari:

Jumla ya watoto 282,000 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Songwe wamepata chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa polio katika kipindi cha kampeni maalumu ya siku nne.

Songwe. Jumla ya watoto 282,000 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Songwe wamepata chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa polio katika kipindi cha kampeni maalumu ya siku nne.

Katika Kampeni hiyo iliyoanza Mei 18 hadi Mei 21 mwaka huu, timu ya wataalamu walikuwa wakipita nyumba kwa nyumba katika vijiji na mitaa mbalimbali na kuwachanja watoto hao.

Mratibu wa chanjo mkoani hapa, Moses Lyimo amesema katika kampeni hiyo jumla ya watoto 282,000 ambao ni sawa na asilimia 126 ya lengo la kuchanja watoto 242,452 wamechanjwa na kwamba mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na wazazi wanaotambua umuhimu wa kuwakinga watoto wao.

Lyimo amesema pamoja na kampeni hiyo, watoto waendelee kupata chanjo kwa tarehe walizopangiwa katika kliniki zao na kuwa kampeni nyingine kama hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Juni na Julai mwaka huu.


Mmoja wa wazazi Yasinta Mwalembe mkazi wa Iganduka wilayani hapa amesema amejitokeza kuchanja watoto wake wawili kwa hiari kutokana na elimu ambayo amekuwa akiipata na kuwa anaamini chanjo hizo zipo miaka mingi na hajaona madhara yoyote.

"Nawasihi wazazi wenzangu ambao wanahusianisha chanjo hii na chanjo ya Uviko-19 kuacha fikra hizo bali wahakikishe wanawachanja watoto wao ili wapate kinga dhidi ya polio" amesema Yasinta.