SportPesa yaibuka na mshiko deile

SportPesa yaibuka na mshiko deile

Muktasari:

  • Kampuni ya SportPesa ni miongoni mwa wadhamini wakubwa wa klabu kongwe nchini za Simba na Yanga.

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa wamezindua kampeni maalumu ambayo wateja wake watakuwa na nafasi ya kubashiri na kushinda mamilioni kwa mechi za mwezi huu wa Juni, 2021.

Mchongo huo mpya kwa umezinduliwa rasmi leo Alhamisi ya Juni 10, 2021 jijini Dar es Salaam na utahusisha kampuni za simu za Tigo, Vodacom na Airtel.
Hatua hiyo inalenga kuwazawadia wateja hasa katika kipindi hiki cha mechi za Fainali za Mataifa Ulaya (Euro 2020) pamoja na michezo mingine ikiwemo Copa America na Ligi Kuu Bara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa, Sabrena Msuya amesema kuwa katika kipindi hiki wameona wawazawadie wateja wao kupitia mchongo huo wa “Mshiko Deilee”.

“Promosheni hii inaanza rasmi kesho Juni 11, 2021 na itafikia mwisho Julai 11, 2021. Kutakuwa na washindi 30 kila siku ambao watajishindia kuanzia Sh 10,000 kila mmoja. Pia, kutakuwa na zawadi ya Sh1 milioni kwa wiki kwa washindi watatu na mwisho kutafanyika promosheni kubwa ambayo mshindi ataondoka na Sh15.8 milioni.
“Droo zitachezwa kila siku na washindi watatangazwa kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii zikiwemo za washirika wetu,” amesema Msuya.
“Napenda kuwakaribisha watumiaji wa mitandao yote kushiriki kwenye promosheni hii hata wale ambao hawajajisajili na SportPesa ili waweze kushinda zawadi za kila siku.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Tigo, Fabian Felician amesema: “Katika msimu huu wa mechi za Euro na zinginezo tumeona ni vizuri kushirikiana na SportPesa ili wateja wetu wa Tigo Pesa waweze kubashiri kwa urahisi na kupata nafasi ya kujishindia mamilioni ya pesa”

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa M-Pesa, Kelvin Nyanda amesema mbali ya kuwa ligi hii ni ya muda mchache, lakini itawapa fursa watumiaji 10 kila siku kujinyakulia pesa.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wanamichezo kushiriki mara nyingi wawezavyo, maana ushindi upo kwa ajili yao sababu ya “Mshiko Deilee,” amesema.