Takukuru kuajiri watumishi wapya 322

Mkurugenzi wa Takukuru Salum Rashid Hamduni akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Takukuru Kiteto leo Mei 5, 2023 jengo ambalo limegharimu sh 192mil. Picha na Mohamed Hamad Kiteto

Kiteto. Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Rashid Hamduni, mesema amepata  kibali cha kuajiri watumishi wengine wapya 322 ili kuongeza jitihada za mapambano ya Rushwa nchini.

Hamduni ameyasema hayo hapa leo Mei 5 2024; wakati akizindua jingo la taasisi hiyo lililogharimu kiasi cha Sh192 milioni na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa utashi wake na Serikali kuwezesha chombo hicho kupata rasilimali fedha na watu katika mapambano dhidi rushwa.

"Tuendelee kuishukuru Serikali ya awamu ya sita, tumepata Kibali cha kuajiri watumishi wengine 322 hapa nchini na wataanza kupata mafunzo...nitoa ahadi kilio cha upungufu wa watumishi kitapungua tutawaleta katika wilaya na kutoa kipaumbele kwa kuzingatia ukubwa wa wilaya hii ya Kiteto na nchi nzima kwa ujumla," amesema.

Kwa mujibu wa bosi huyo wa Takukuru, kazi ya kupiga vita rushwa si kazi ya mtu mmoja au tasisi Fulani bali ni kazi ya umma wote wa Tanzania, hivyo ni vema watu wote wakahamasika na hivyo kujenga tabisha ya kushiriki vita hiyo

Akizungumzia mradi wa ujenzi huo Dk. Emmanuel Kiyabo, Mkurugenzi wa usimamizi miliki ametaja gharama za mradi huo kuwa ni Sh192 milioni huku Suzan Raymond Mkuu wa chombo hicho Mkoa wa Manyara akiahidi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.

"Mradi ulikamilika toka Novemba 6.2022 ikiwa ni ongezeko la wiki sita kutoka katika makadirio ya awali ya muda wa mradi na ulitumia kiasi cha Sh192 milioni,"alisema Kiyabo.

Susan yeye anaamini jingo jipya walilopata litaleta chahcu katika utendaji wao: “Kupatikana kwa Jengo hili jipya litaleta chachu na ari mpya ya kufanya kazi hivyo tuna ahidi kwamba tutafanya kazi kwa bidi kwa maslahi ya nchi."

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Fadhili Alexander Kaimu katibu Tawala Wilaya (DAS), amesema wilaya ya kiteto imepata zaidi ya Sh20 bilioni za miradi ya maendeleo hivyo inahitaji jicho pevu katika miradi hiyo.

"Katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia, wilaya ya Kiteto imepokea zaidi ya Sh20 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo, hivyo inahitaji jicho haswa, tena kali la Takukuru ili fedha hizo zibaki salama na zitimize lengo mahususi la Serikari na kuleta tija kwa umma," amesema Alexander.

Naye Mbunge Asia Halamga anayewakirisha vijana, ameipongeza serikali kwa kutoa fedha hizo, lakini pia aliomba kuongezwa kwa watumishi wapya katika tasisi hiyo ambayo pamja na mambo mengine, ina jukumu la kupambana na vitendo vya rushwa nchini.

"Pamoja na kufanya kazi nzuri Takukuru wako katika mazingira magumu sana…Manyara ni kubwa watumizi wako wachache hivyo tunaomba Serikali na Mkurugenzi leo upo hapa ni mara chache sana kupatikana sasa waongezwe," amesema Mbunge huyo.

Nao baadhi ya wananchi wameshukuru kukamilika kwa jengo hilo wakiamini litakuwa msaada mkubwa kwao

"Takukuru ni chombo muhimu kina hitaji msaada mkubwa…kwa sasa wako karibu na wananchi ni waungwana na wastaarabu"alisema Alhaji Mbaruku Saidi

Kwa upande wa Musa Ibrahim mkazi wa Manyara, amesema: “Huko nyuma watu walitesena sana kwa kudhulumiwa haki zao kwa za rushwa, hata hivyo uwepo wa ofisi hii unafanya hata hao viongozi kuwa makini."

Kwa upande wake, Hakimu wa wilaya hiyo Boniphace Lihamwike amesema: “Rushwa ya ngono kwa Kiteto itamalizika kutokana na jengo hili kukamilika, Haya ni maendeleo katika mapambano ya rushwa ni juhudi nzuri zinazofanyika kujenga miundo mbinu na inasaidia sana kuwafanya maafisa wa TAKUKURU kukaribiana na wananchi"