Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takukuru yaanza uchunguzi ujenzi wa soko Tunduma

Muktasari:

  • Kamanda wa Takukuru mkoani Songwe, Endings Mwakambonja amesema miradi 29 inayotekelezwa katika mkoa huo imebainika kuwa na mapungufu hivyo wameanza uchunguzi.

Songwe. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Songwe, imeanzisha uchunguzi katika miradi ya ujenzi wa soko la wamachinga lenye thamani ya Sh.6 bilioni, katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Kamanda wa Takukuru mkoani Songwe, Endings Mwakambonja akitoa taarifa ya miezi mitatu ya taasisi hiyo leo Mei 16, 2023 amewaambia waandishi wa habari kuwa katika kipindi hicho miradi 29 yenye thamani ya zaidi ya Sh19.2 bilioni ilifuatiliwa na kuwa kati ya miradi hiyo 10 yenye thamani ya zaidi ya Sh7.9 bilioni ilibainika  kuwa na mapungufu.

Mwakambonja ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa soko la machinga lililopo kata ya majengo mjini Tunduma ambalo tayari malipo ya awali ya Sh385 milioni yametolewa lakini thamani halisi katika mradi huo haionekani ikiwa ni pamoja na kulipa mkandarasi kiasi chote cha fedha anazostahili Sh62 milioni ili hali kazi haijakamikika jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za uzabuni.

Mwakambonja ametaja miradi mingine ambayo taasisi yake imeanzisha uchunguzi kuwa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Namole kwa thamani ya Sh4 bilioni, huku wakibaini ununuzi wa mabati yenye thamani ya zaidi ya Sh62 milioni bila kufuata taratibu za manunuzi.

"Mradi mwingine ni ujenzi kituo cha Afya Mwaka Kati kwa thamani ya Sh500 milioni ambapo kwenye mradi huu malipo yamefanywa pasipo vifaa kufika eneo la mradi," amesema Mwakambonja.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa Songwe, Dk Francis Michael alifanya ziara ya kustukiza katika soko hilo na kutoridhika na thamani halisi ya ujenzi wake ambapo alisema matumizi ya zaidi ya Sh411milioni hayaendani na thamani ya fedha inayoonekana.