Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanapa: Milioni tano kumpa mnyama jina lako

Muktasari:

  • Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa) limeanzisha utaratibu maalum ambao kwa mtu anayetaka kuasili ama kumpa mnyama jina lake anaweza kufanya hivyo kwa kulipia.

Dodoma. Baada ya wanyama kupewa majina ya watu maarufu wa nje ya nchi, Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania (Tanapa) limeanzisha utaratibu maalum wa kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia Sh5 milioni.

 Utaratibu huo nakuja baada ya baadhi ya wanyama akiwemo simba aliyepewa jina Bob Juniour, faru aliyepewa Faru John na Rajabu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 24, 2023 na Kamishina wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2023/24.

“Tumeanzisha utaratibu wa kuwapa majina baadhi ya wanyama lakini sio bure. Na hawa wanyama sio wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako,”amesema.

Amesema bodi ya menejimenti ya Tanapa imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.

Pia amesema mtu yoyote ambaye anataka aendelee kumuona anaweza kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh1 milioni kila mwaka.

Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya faru pia wana majina akiwemo yeye mwenyewe ambaye mmoja wa faru katika Hifadhi ya Serengeti amepewa jina lake.


Aelezea asili ya Bob Junior

Kuhusu simba aliyepewa jina la Bob Juniour, Kamishna Mwakilema amesema jina hilo alipewa na waongoza utalii baada ya kulinganisha mnyama huyo wakamlinganisha na Bob Marley ambaye alivyokuwa na rasta zake nyingi, ukubwa na kivutio kwa watalii.

“Bahati mbaya jina hilo halikutambulika hadi alipokuja kufa akaanza kuvuma kuwa Bob Junior amekufa,”amesema.