Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanroads Mbeya yafunga taa za kidijitali kusaidia wanafunzi kuvuka barabara

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya (RTO), Notker Kilewa akiongoza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki (CUoM),namna kuzingatia matumizi ya taa za watembea kwa miguu. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya usalama barabarani yatakayojumuisha  upanuzi wa barabara na uwekaji wa taa zaidi, kufuatia kukithiri kwa ajali  zinazo gharimu maisha ya wanafunzi wakati wa kwenda na kutoka shuleni.

Mbeya. Kufuatia ajali zinazohusisha wanafunzi, Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mbeya umefunga taa za kisasa za kidijitali katika maeneo ya Igawilo, Uyole na karibu na Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya (CUoM) kwa lengo la kuongeza usalama wa watembea kwa miguu, hususan wanafunzi.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mbeya, Suleman Bishanga, amesema hayo jana Juni 6,2026 hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha usalama barabarani katika maeneo yanayotumiwa na wanafunzi kuvuka kwenda na kutoka shule.

Amesema mfumo huo utamwezesha mtumiaji kubonyeza kitufe kabla ya kuvuka barabara, ambapo taa zitatoa ishara kwa madereva kusimama ili kuruhusu watembea kwa miguu kuvuka kwa usalama.

Bishanga amesema Tanroads pia inapanga kuboresha miundombinu ya eneo hilo, ikiwemo mabega ya barabara na taa za barabarani, huku akiwataka wananchi kushiriki kulinda miundombinu hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, Notker Kilewa, amepongeza hatua hiyo akisema itachangia kuimarisha usalama wa wanafunzi na watumiaji wengine wa barabara.

Wanafunzi  wakivuka barabara kwa kutumia kivuto cha taa za kisasa katika eneo la Bima Uyole Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Baadhi ya wanafunzi na wakazi wa eneo la Igawilo wameipongeza Serikali kwa uwekaji wa taa hizo na kuomba elimu zaidi kuhusu matumizi yake pamoja na kuimarishwa kwa usimamizi wa sheria za usalama barabarani katika eneo hilo.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Hasanga wameishukuru Serikali kwa kufunga taa hizo, wakisema zitasaidia kupunguza hatari ya kugongwa na magari wakati wa kuvuka barabara.


"Eneo hili ni hatari kwetu. Wanafunzi kadhaa wamewahi kupata ajali licha ya kuwepo kwa kivuko. Tunaomba tuendelee kupewa elimu kuhusu matumizi ya mfumo huu mpya," amesema mmoja wa wanafunzi hao.


Naye Mkazi wa Igawilo, Uyole, Sekela Joel, ameomba askari wa usalama barabarani kuweka ulinzi wa mara kwa mara katika eneo hilo ili kudhibiti madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.


"Asubuhi na jioni watoto wanapata changamoto kubwa kuvuka barabara. Tunaomba polisi wawepo mara kwa mara kwa sababu baadhi ya madereva husababisha ajali na kutoroka," amesema.