Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kinara anuani za makazi Afrika

Mratibu wa utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi nchini, Jampion Mbugi

Morogoro. Asilimia 95 ya utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi nchini zimeifanya Tanzania kuwa kinara kwa Bara la Afrika ikilinganishwa na nchi nyingine tangu kuanza kwa program hiyo mwaka 2010.

Mratibu wa utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi nchini, Jampion Mbugi alitaja mafanikio hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya watendaji kata, wenyeviti wa Serikali za Mitaa na wakusanyaji taarifa kuhusu utekelezaji wa mfumo za anuani za makazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Mfumo wa anuani za makazi utekelezaji wake hususani kwa nchi za Bara la Afrika ulianza 2010 ambapo nchi nyingi za Afrika zilianza jitihada miaka hiyo, utekelezaji huo kwa Tanzania kwa mujibu wa mpango kazi ulitakiwa kukamika 2015, lakini ilipofika 2015 kwa Tanzania ilikuwa asilimia 2 tu.

Mbugi amesema mwaka 2021 Tanzania utekelezaji ulifikia asilimia 3 tu na si kwa Tanzania tu na nchi nyingi za Afrika utekelezaji ulikuwa wa kusuasua,na kwamba kwa sababu utekelezaji wa anuani hizo za mfumo wa makazi ni mtambuka unahitaji ushirikishwaji wa wadau mbalimbali kwani mfumo wenyewe ni mgumu kwa sababu kila nyumba, mtaa, na barabara zinapaswa kufikiwa.

“Ilipofika Mei 2022 utekelezaji wake uliweza kufikia zaidi ya asilimia 95 kwa sababu maeneo mbalimbali kila nyumba, barabara na kila mtaa ziliweza kufikiwa, sasa kufatiwa oparesheni hiyo ndio iliyotusukuma kuonekana kuwa vinara barani Afrika, na ndio maana tunajivunia jitihada zilizoanzishwa na Rais,”amesema.

Amesema kuwa Tanzania haiwezi kuingia kwenye uchumi wa kidigitali bila kuwa na miundombinu ya utambuzi kwa sababu uchumi huo unajumuisha ufikishaji wa barua, vipeto na kila kitu pamoja na huduma nyingine za majumbani.

Mbugi amesema kama nchi ina fursa ya kuingia kwenye uchumi wa kidigitali na nchi kuweza kunufaika na masuala mbalimbali ya ufikishaji wa huduma na urahisishaji wa huduma zote kwa ujumla.

“Ukienda nchi nyingi za Afrika utekelezaji wake umefikia asilimia tatu, asilimia 15 na karibuni nchi zote hazijaweza kufikia Tanzania, lakini bado tunaangalia nchi nyingine zinafanyaje, kila nchi inaweka mfumo wa utambuzi kulingana na malengo yake, mfumo wetu kwa Tanzania umejumuisha masuala mbalimbali yakiwemo ya usalama, ulinzi, biashara mtandao,”amesena.

Akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Rebecca Nsemwa, Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro, Hillary Sagala, amesisitiza Jamii kutoharibu alama za anuani za makazi, ambapo baadhi ya maeneo vimeondolewa hali ambayo inakwamisha jitihada za Serikali.

Hillary amesema Serikali inaendelea kutoa Elimu ya kuongeza uelewa kwa jamii namna ya kuthamini miundombinu hiyo ambayo imetumia kiasi kikubwa cha fedha kukamilisha utekelezaji wake.

Washiriki 1,200 wanaotarajiwa kufanya zoezi la uhakiki wa anuani za makazi kwa siku 14 Manispaa ya Morogoro.